Ticker

6/recent/ticker-posts

RIDHIWANI KIKWETE AFANYA KAMPENI ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANANCHI WA JIMBO LA CHALINZE



Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.
 Wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Kijiji hicho ili kuweza kumsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani).
 Diwani wa Kata ya Mbwewe,Omari Mhando akisisitiza jambo kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwamuhombo wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani) uliofanyika leo Machi 16,2014 kwenye Uwanja wa Kijiji hicho.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akipiga stori na vijana wa Kijiji cha Kwamduma.

Post a Comment

0 Comments