Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti ya Mtanzania.
Mwandishi Wetu, Moshi
MAGARI yanayofanya safari zake
katika Barabara ya Moshi-Arusha zimegoma kufanya safari kwa takribani masaa 9 yakipinga
kulipishwa bondi ya makosa ya shilingi elfu 30 katika kila kituo kwa kosa lilelile.
Wakizungumzia chanzo cha mgomo
huo, baadhi ya wamiliki na madereva wa magari yaendayo, Marangu, Rombo, Arusha,
Rau pamoja na magari yote yanayotoa huduma katika maeneo ya mijini kama vile
pasua KCMC na Uru, wamesema sababu ya msingi ya kufanya mgomo huo kulishinikiza
kitengo cha usalama barabarani na Mamlaka ya usafiri wa majii ya nchi kavu (SUMATRA),
kuangalia upya tozo hizo.
Akizungumza kwa niaba ya madereva
hao, katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, na kukutanisha pande zote kwa
maana ya Akiboa, Jeshi la Polisi na SUMATRA, Mwenbyekiti wa Akiboa kanda ya Kaskazini,
Hussein Mrindoko, amesema kiini cha mgomo huo ni kitendo cha udhalilishaji
wanaofanyiwa na askari wa usalama barabarani.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo
kidogo cha polisi Moshi mjini OCS, Hendry Nguvumali anayelalamikiwa kulazimisha
faini kinyume cha sheria, pamoja na kufanya kazi akiwa mlevi amesema malalamiko
yote yametokana na ukweli kwamba anafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jeshi la
polisi.
Akijibu malalamiko yaliyolekezwa
kwa SUMATRA kuhusu ucheleweshaji wa stika na ukamataji wa leseni za biashara ya
usafiri, Meneja wa mamlaka hiyo mkoa Kilimanjaro Fabian Nyang’oro amesema SUMATRA
imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa taratibu na sheria za usalama
barabarani pamoja na sheria ya umiliki wa vyombo vya usafiri.
Amesema endapo mmiliki wa Chombo
cha biashara ya usafiri atakiuka sheria
hizo wao kama wasimamizi kazi yao sio kukamata magari bali kuhakikisha stika
ambazo zimechukuliwa kinyume cha taratibu wa utoaji wa leseni za biashara
zinafutwa.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Leonidas Gama, alisema kimsingi tatizo hilo halikutakiwa kuwepo maana taratibu
zote za kisheria ziko wazi ambapo aliitaka SUMATRA kama wenye dhamana kuu na
usafiri barabarani kuhakikisha wanakaa meza moja na Jeshi la Polisi pamoja na
Akiboa kuzungumzia malalamiko yote yaliyowasilishwa na kuyapatia ufumbuzi.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi
mkoani hapo, Robert Boaz, aliwataka Madereva kufuata sheria na kuwataka kuacha kulalamika
ambayo kimsingi wanayasababisha wao kutokana na kukiuka taratibu za usalama
barabarani.
Amesema baada ya kutolewa kwa
taarifa ya Mkoa wa Kilimanjaro kuwa ya pili kwa ajali za barabarani, Jehsi la
Plisi mkoani hapo lilichukua hatua ya kuhakikisha inakabiliana na tatizo hilo
ambalo alisema kwa asilimia kubwa husababishwa na uzembe wa madereva wawapo
barabarani.
|