msafara wa katibu wa ccm wialya ya Arumeru Gpdfreu Sabuni ukiwa unawasili katika kijiji cha ilikiushing katika mkutano wa adhara
wamama wa msanja wakiendelea kuserubuka katika mkutano huo
vijana wakiendelea kuserubuka katika kijiji hicho
katibu wa vijana wilaya ya arumeru akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema
picha ikionyesha baadhi ya wanachama wa liojiunga na ccm wakila kiapo katikati ni aliyekuwa mwenyekiti vijana chadema kata ya orturumenti Thomasi Kivuyo
mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkoano kwa katibu wa siasa uenezi JOnasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm
Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya wananchi 100 wa kata ya ortumunti wilyani Arumeru kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani wamehamia chama cha mapinduzi akiwemo
mwenyekiti wa vijana wa chadema kata hiyo .
tukio hilo lilitokea juzi wakati wa mkutano wa adhara wa chama cha
mapinduzi uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru
mkoani hapa.
Akiongea wakati wa kurudisha
wa kurudisha kadi ya chadema na kukabidhiwa kadi ya ccm mwenyekiti wa
vijana wa chadema Thomasi Molel alisema kuwa
ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kuoana kuwa tangu awe katika
chama cha chadema ajapata faida yeyote wala ajaona kitu ambacho wananchi
wanafaidika kupitia chama hicho.
Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia
katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo hivyo ameamua kuondoka
katika chama hicho kwani chadema ni chama ambacho akina democrasia ya
kweli ambayo inatakiwa iwenacho kama
chama
Alisema kuwa viongozi wengi wa chadema wamekuwa wanatoa
ahadi za uongo kwa wananchi na mbali na
hicho pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa
anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atake weza
kukisemea chama .
Aidha alibainisha kuwa katika kata yao tangu upinzani wameingia madarakani hamna
kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha
wananchi hela nyingi bila kufanya
maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa
kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea
shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa
Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato
na matumizi ya kata yao tofauti na
kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.
Kwa upande wake
katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na
pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na
matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda
katika ofisi ya mkurugenzi kufuatilia
swala hili.
Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi
kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya
kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka na kata yao haitapata viongozi wazuri.
Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana
mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao
na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto
wao wakilala njaa