MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, amewaagiza watendaji wa
vijiji, mitaa na kata kuhakikisha wanatunza na kulinda vyanzo vya maji
ikiwemo miundombinu yake ili kuwepo na uhakika wa maji.
Dendegu alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa semina kwa
wenyeviti wa vijiji, mitaa na kata walioko jijini humo iliyoandaliwa na
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) iliyofanyika
Mowe kwenye Kata ya Pande.
Alisema ili huduma ya maji safi na salama iweze kuwa endelevu ipo
haja ya kulinda vyanzo vyake na miundombinu isiharibiwe, kwani mabalozi
wa karibu ni viongozi hao sababu ndio wapo karibu na wananchi wengi.