DIWANI NANYARO ATOA MSAADA WA CHAKULA

DIWANI wa Levelosi, Ephata NanyaroDIWANI wa Levelosi, Ephata Nanyaro (CHADEMA), ametoa msaada wa unga, mahindi na sukari kwenye Shule ya Msingi Levelosi ili kuwawezesha wanafunzi kupata uji nyakati za mchana baada ya serikali kushindwa kuwapatia chakula wawapo shuleni.
Nanyaro alitoa msaada wa sukari kilo 105 na unga wa mahindi kilo 220  juzi  na kukabidhiwa kwa mwalimu wa chakula, Frida Malya, mbele ya  Mwalimu Mkuu, Elisante Kaaya,  walimu wengine na wanafunzi wa shule hiyo.
Alisema ataendelea na utaratibu wa kupeleka msaada kama huo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata uji kwa kipindi chote cha mwaka, jambo alilosema litasaidia kuwapunguzia wanafunzi njaa.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia