Maandalizi
ya mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge kupitia CCM jimbo la
Chalinze yaendelea vizuri ambapo jioni ya leo Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajiwa kuhutubia wakazi wa Chalinze na
Vitongoji vyake pamoja na kumnadi mgombea wa ubunge kupitia CCM Ndugu
Ridhwani Kikwete.
Barabara
Kuu iendayo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha ikiwa imependeza kwa
bendera za CCM ,ambapo masaa machache yajayo kutakuwa na mkutano mkubwa
wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge CCM.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mratibu wa Kampeni za Ubunge
Jimbo la Chalinze akisoma vichwa vya habari vya magazeti ya leo kwenye
moja ya vibanda vya magazeti Chalinze huku sehemu kubwa ya maeneo yote
yakiwa yamebandikwa mabango yenye picha za mgombea kiti cha ubunge
kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
Mratibu
wa Kampeni za Ubunge CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye akibadilisha na
Kamanda waVijana mkoa wa pwani wakati wa kukagua hatua za mwisho za
maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa Kampeni.
Shumina
Sharif Kiongozi wa kampeni kata ya Msata na Mjumbe wa mkutano mkuu CCM
Taifa akiwa na mratibu wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze
Nape Nnauye wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya mkutano wa
ufunguzi wa kampeni jimbo la Chalinze.
Mratibu
wa Kmapeni za Chalinze CCM Nape Nnauye akijadiliana jambo na maofisa wa
Chama Cha Mapinduzi wakati wa maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa
kampeni za CCM jimbo la Chalinze.