Timu ya AFC
ya Arusha wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa wa Arusha baada ya kuifunga timu
ya laibon ya longida kwa magoli 9-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya sita
bora ya ligi ya mkoa wa Arusha.
Ushindi huo
umeifanya Timu ya AFC kufikisha jumla ya pointi 11 sawa na mana FC lakini afc
ikanufaika na idadi kubwa ya magoli kwa kuwa na magoli 17 ya kufunga na matatu
ya kufungwa wakati mana wao wana magoli tisa ya kufunga na hawajafungwa goli hata
moja
Katika
mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sheikh amri abeid kaluta
mjini hapa hadi mapumziko afc walikuwa wanaongoza kwa magoli 4-0 yaliyofungwa
na Eriki Daudi na Jamal aliyefunga
mawili na Mgona Kifaru
kipindi cha
pili afc walikuja na nguvu zaidi na kujipatia magoli matano zaidi yaliyofungwa
na Alidina Hashim kwa penalt,Samson Mwalukwa,Abas Nkuba na Jamal tena
aliyefunga magoli mawili.
nafasi ya
pili imeshikwa na mana FC ,wa tatu Arusha meat,wa nne flamingo,nafasi ya tano
imeshikwa na suye na timu iliyoshika mkia ikiwa ni timu ya laibon ya Longido.
mgeni rasmi
katika mchezo huo alikua mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa Sabi
aliwazawadia kombe afc ambao sasa watauwakilisha mkoa wa Arusha katika ligi ya
kanda ngazi ya taifa
kwa kutwaa
ubingwa huo afc imezawadiwa shilingi million 50 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Arusha
Magesa Mulongo ambaye aliahidi kutoa kiwango hicho kwa timu yeyote itakayotwaa
ubingwa wa mkoa huku wadau wa michezo wa mkoa wa arusha wakiahidi kuiunga mkono
timu hiyo ili ipande daraja hadi kufikia ligi kuu kama zamani.
Munasa
alisema kuwa kiwango cha wachezaji kinaridhisha ila kwa sasa bado upande wa
makocha bado hawatoshi ambapo ameahidi kuanza mchakato wa kutafuta makocha
kutoka nchi za nje watakaokuja kuwanoa makocha wa Arusha.
Tags
MATUKIO MICHEZO