Bondia Fracis
Cheka amejigamba kambi aliyoweka jijini Nairobi nchini Kenya imemuongezea
kujiamini kuelekea pambano lake la ubingwa wa dunia dhidi ya bondia valain
ludov kutoka Russia
Akizungumza
na LIBENEKE LA KASKAZINI BLOG mjini hapa akiwa safarini kuelea Dar-es-saalam kutokea
Nairobi cheka amesema kuwa kwa kuweka kambi Nairobi amejijenga kisaikolojia na
pia mazoezi aliyoyapata kutoka kwa mabondia wa Kenya yamemuongezea mbinu
hususani za kupambana na mabondia warefu.
“nimejifua
kwa nguvu za kuongezewa mbinu na kocha wangu Abdala Salehe ‘comando’ mazingira
yalikuwa mazuri nina kila sababu ya kujivunia mazoezi niliyopata nikiwa
Nairobi”alisema Cheka.
Cheka alisema
kuwa mabondia wengi wa Kenya ni warefu tofauti na wa Tanzania ambao wengi ni
wafupi na hali ya hewa ya Nairobi ni nyepesi inayoruhusu kufanya mazoezi mazito
na kwa muda mrefu na kwa sasa anajiona yuko tayari kumvaa mrusia huyo.
Cheka
aliwahakikishia mashabiki wake na wadau wa ngumi hapa nchini kufanya vizuri
katika pambano hilo hivyo wakae mkao wa kula kwani katika pambano hilo
anatarajia kuiletea nchi yetu heshima kwa pambano la ngumi.
“Mashabiki
wakae mkao wa kula na waje kuona namna ntakavyomchakaza huyo mrusia kwani najua
kushinda kwangu kutailetea hata nchi yangu heshima na wadau wa ngumi watapata
furaha kuona ushindi unabaki nyumbani” Alijitamba Cheka.
Pambano hili
ka ubingwa wa dunia linalotambuliwa na IFB litafanyika jijini dare s salaam
April 5 na maandalizi ya jumla kwa bondia Francis Cheka yamekamilika asilimia
mia moja kama alivyoelezea.
Cheka aliyekuwa
ameambatana na kocha wake Abdala Salehe ‘comando’ alipitia mkoani arusha ambapo
alipumzika kwa muda mfupi kabla ya kuendelea na safari yake.
Cheka pia
alibahatika kuona mazoezi ya mabondia wa mkoani Arusha ambao walikuwa wanafanya
mazoezi kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sheikh amri abeid mjini hapa.