BREAKING NEWS

Tuesday, March 4, 2014

LORD EYEZ ASIMAMISHWA KWENYE KUNDI LA "WEUSI" BAADA YA KUKAMATWA NA TUHUMA ZA WIZI JIJINI ARUSHA, NIKKI WA PILI ATOA TAMKO


Msanii na msemaji mkuu wa Weusi Nikki wa Pili, ametoa tamko juu ya msanii mwenzao Lord Eyes na kusema kuwa kampuni kama kampuni imemsimamisha Lord Eyes na kwa yeyote anaetaka kujua habari zake amtafute Lord mwenyewe.


"Tamko ni kwamba Lord Eyes amemsimamishwa kazi, kampuni imemsimisha kazi, kwahiyo kuanzia sasahivi habari zote za Lord Eyes ataziripoti Lord Eyes mwenyew, sababu za kumsimamisha ni za ndani ya kampuni kwahiyo hatuwezi kuzitoa. Kampuni yoyote inamisingi yake ambayo inafanya maamuzi.kwa mamlaka ya kampuni hatuwezi tena kumzungumzia Lord Eyes, kwasasa hivi yeye sio member wa Weusi amesimamishwa mpaka hapo tutakapotangaza upya kumrudisha. Kwahiyo taarifa za Lord Eyes ni zake sio za Weusi tena" amesema Nikki wa Pili.

Katika U Heard ya jana, mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rose amedai kuwa Mume wake ambae alikuwa nae siku ya tukio anaeitwa Eli Furaha aliiibiwa lapto kwenye gari walilokuwa wamepaki maeneo ya njiro. "sisi tulikuwa tumepaki gari siku ya ijumaa jioni yeye alikuwa na wenzake kama wanne hivi, wakaspray kioo cha gari, kikawa chengachenga halafu wakaiba laptop jioni. sisi tulimuona kabisa kwa macho aliingia na wenzake wakaagiza vinywaji wakanywa na sisi tukala, kwahiyo wakatoka wao wakatuacha sisi ndani, ile kutoka tu kama dakika tano na sisi kutoka nje tayari gari wameshavunja. sasa tukaja polisi tukaripoti, tukaendelea kumtafuta, juzi saa 11 ya asubuhi ya jumapili lakini yupo polisi sasa hivi.Laptop bado hatujaipata ndio polisi wanambana lakini bado anakataa kwamba sio yeye." amesema Rose

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates