WITO KWA WANANCHI KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA NA KUIMARISHA NIDHAMU YA USAFIRI




Na Woinde Shizza, Arusha

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha,  Joseph Modest Mkude, amewataka wananchi kujiunga na bima ya afya, kudumisha nidhamu katika usafirishaji, na kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya kijamii, wakati wa zoezi la ugawaji pikipiki kwa vijana wa bodaboda.

Ameyasema hayo hii leo katika viwanja vya makumbusho jiji hapa wakati mkuu wa wilaya ya Arusha  akizungumza na waendesha bodaboda wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoji wa pikipiki za mikopo chini ya udhamini wa Benki ya Azania.

Amewataka waendesha pikipiki hao kuhakikisha wanachangamkia fursa hiyo ya kupata mkopo wa pikipiki na mwisho kuwa wamiliki kamili wa pikipiki zao za biashara yao huku akisisitiza  nidhamu ya matumizi ya fedha ili waweze kuwa waaminifu na kurudisha mikopo hiyo kwa Muda 


  
“Tusisimame tulipo, bali tuendelee mbele ,ni lazima tushirikiane katika kila hatua, hasa katika miradi ya afya na usafi wa mazingira na nisisitize mshikamano na ushirikiano katika miradi ya kijamii ni msingi wa maendeleo endelevu” alisema.

" kujiunga na bima ya afya ni hatua muhimu, kwani husaidia kila mwananchi kupata huduma bora za matibabu bila gharama kubwa ,Sasa ni wakati wa kila mmoja kuanza na bima ya afya Tukikusanya nguvu, tutakuwa imara zaidi kama jamii,” aliongeza.

Mkude pia aliwaonya baadhi ya vijana wanaojihusisha na biashara ya pikipiki zisizo rasmi,na kuwataka kuhakikisha wanazingatia taratibu na sheria ili kulinda usalama wa watumiaji na taswira ya sekta ya usafirishaji.

Aidha pia alipongeza nidhamu, mshikamano, na ushirikiano wa bodaboda, akiahidi kuendelea kushirikiana nao kuhakikisha sekta hiyo inabaki salama na yenye tija kwa wananchi huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia sekta hiyo kikamilifu, na kubainisha kuwa wanataka kuona vijana wakitumia ajira hii kwa uadilifu, usalama, na utii wa sheria


kwa upande wake katibu wa bodaboda Wilaya ya Arusha mjini  Richard Magembe, alishukuru sana serikali  kwa namna inavyotambua mchango wa kundi la bodaboda katika kukuza uchumi wa wananchi  na kusema kuwa wapo tayari kushirikiana nayo na wadau wengine wakati wowote watakapohitajika.

Aidha alibainisha mafanikio yao, ikiwemo kupata shilingi milioni 20 kutoka kwa wadau wa maendeleo zilizotumika kuanzisha shughuli za kiuchumi na kuboresha ustawi wa wanachama, pamoja na kufungua akaunti katika kata zote 25 za Wilaya ya Arusha Mjini kuhifadhi michango na akiba.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa wito wa mshikamano, uwajibikaji, na mshikamano miongoni mwa wananchi, huku viongozi wa serikali na wadau wa usafirishaji wakiahidi kushirikiana zaidi katika miradi ya maendeleo ya kijamii.









About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia