Na Woinde Shizza,Arusha
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter Mtwale, amewataka viongozi wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo ya taasisi hiyo.

Akizungumza Aprili 23, 2026 jijini Arusha baada ya kutangazwa kwa matokeo ya nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, Mtwale alisema ushindi wa viongozi hao unaonesha wazi imani kubwa waliyopewa na wajumbe, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, uwajibikaji na uadilifu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi huo, Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine Sima, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa ALAT Taifa baada ya kupata kura 273 kati ya kura 339 zilizopigwa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha alishika nafasi ya pili kwa kura 45, huku Seif Hassan Daud akimaliza katika nafasi ya tatu kwa kura 17.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Agneta Mpangile aliibuka mshindi kwa kupata kura 189 kati ya kura 337 zilizopigwa, akifuatiwa na Ali Sadiki Mkaingwa aliyepata kura 118, na Solomon Mabati aliyepata kura 29.
Aidha, uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT Taifa umefanyika, ambapo matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa kesho
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia