RC MAKALLA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA GAVANA WA ISTANBUL, NCHINI UTURUKI

 




Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla na ujumbe wa Tanzania amekutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Instabul Nchini Uturuki Mhe. David Gul.


Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kudumisha ushirikiano miongoni mwao kwa maslahi na ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.


Mhe. Makalla aliyeambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Nguvila, amekuwa nchini Uturuki pamoja na Wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la dunia IPU ikiwa ni maandalizi ya Mkutano ujao wa Jumuiya ya Mabunge duniani, mkutano utakaofanyika Mkoani Arusha mwezi Oktoba, 2026.



About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia