WATENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI WAPATIWA MAFUNZO ARUSHA KUIMARISHA UWEZO WAO

 

baadhi ya watengeneza  maudhui (content creators) mtandaoni wakiendelea kufatilia mada mbalimbali katika mafunzo ya awamu ya kwanza kwa ajili yao yanayofanyika mkoani Arusha yaliyoandaliwa wizara ya habari ,utamaduni sanaa na michezo 




Na Woinde Shizza,Arusha

Watengeneza  maudhui nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha, kuweka akiba, kusimamia vyema miradi yao pamoja na kujifunza elimu ya uwekezaji ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo wanayopata kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa

Wito huo ulitolewa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Sanaa, Utamaduni na Michezo CPA Nyakaho Mahemba, wakati wa mafunzo kwa watengenezaji maudhui 'content creators' mkoani Arusha, yaliyofanyika kwenye Hoteli Corido Spring Aprili 08,2026.

Washiriki hao wamehimizwa kuzingatia matumizi ya lugha za kigeni ili kupanua soko la kazi zao kimataifa, kuzingatia maadili ya Kitanzania, kujifunza tabia za wanyama wanapozalisha maudhui, pamoja na kulinda taarifa binafsi kabla ya kuyachapisha.

 Aidha amesisitiza kuwa, Wizara ya Habari, Mishezo, Sanaa na Utamaduni kupitia mfuko huo, haina upendeleo katika utoaji wa mikopo ukiwa na lengo la kuwawezesha watengenezaji maudhui kuinuka kiuchumi kupitia sanaa na vipaji vyao hivyo elimu ya fedha, inahitaji kuwa na utamaduni wa kuweka akiba na kurejesha mikopo kwa wakati ili kukuza taaluma ya sanaa na kuifanya kuwa chanzo endelevu cha ajira na kipato.

“Mfuko wa Utamaduni na Sanaa unatoa mikopo ili kuwawezesha wasanii na watengenezaji maudhui kukua kiuchumi, hivyo ni muhimu kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwapa nafasi wengine kunufaika pia,” . Amebainisha CPA Mahemba

Naye Mhandisi Benezeth Kabundugur,  kutoka Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia aliwataka watengenezaji maudhui kutumia majukwaa yao ya kidijitali kuhamasisha mabadiliko chanya katika jamii, hususan matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesisitiza kuwa, wanayo nafasi kubwa ya kuelimisha na kuhamasisha jamii matumizi ya nishati safi kwa mbinu zenye mvuto kama video fupi, vichekesho, hadithi na simulizi za maisha halisi ili kufikisha ujumbe kwa ufanisi.

"Mhe. Rais Dkt. Samia ni kinara wa ajenda ya nishati safi ya kupikia barani Afrika, muungeni mkono kwa vitendo ili kufanikisha lengo la kitaifa la kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034"Amesema Kabundugur.

Awali, Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, huku Wizara ya Nishati ikiwa miongoni mwa wadhamini wakuu pamoja na Benki ya CRDB.










About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia