Ticker

6/recent/ticker-posts

PPF WAKABIDHIWA RASMI JENGO JIPYA LA KISASA WALILOJENGA JIJINI ARUSHA LENYE THAMANI YA BILIONI 32.5


Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo,  Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.



DG William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji, idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe. 

Jengo hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani ya jengo.

Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika. 

Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo


Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.

Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara. 

Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C (EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB. 


Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa


Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF Bw..


Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo Ruhasha (kulia) akishuhudia makabidhiano rasmi ya jengo jipya la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo

Post a Comment

0 Comments