MAGONJWA YA MIFUGO ,MAJANGA YA MOTO NI CHANGAMOTO KUBWA INAYOIKABILI HIFADHI YA MKOMAZI





Waandishi wa habari wakiwa wanamuangalia mnyama aina ya kobe aliopo ndani ya hifadhi ya mkomazi
Na Woinde Shizza,Same

Vita dhidi ya magonjwa ya mifugo ,majanga ya moto ,ongezeko la watu pamoja na ukame  ni changamoto kubwa inayoikabili hifadhi ya taifa ya Mkomazi ilipo wilayani same Mkoani Kilimanjaro ambapo imesababisha baadhi ya wanyama ambao ni vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo kutoweka  .



Hayo yamebainishwa na afisa utalii mwandamizi  wa hifadhi ya mkomazi   Pellagy Marandu wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya hifadhi hiyo.



Alisema changamoto hizo zimekuwa zinaletwa na wafugaji ,wakulima ambao wamekuwa wanaleta wanyama ndani ya hifadhi ambapo alibainisha kuwa wanyama wengine wanaweza wakawa na magonjwa ya kuambukiza hivyo wanapoingia ndani ya hifadhi wanaweza kuambukiza wanyama walioko hifadhini hali ambayo inaweza kusababisha janga kubwa kwa hifadhi.

“kwa upande wakulima wamekuwa wakileta madhara wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo ambapo wamekuwa wakiaribu mazingira kwa kuchoma moto mabaki ya mazao ambayo walipanda msimu uliopita “alisema Marandu



Aidha ilikukabiliana na changamoto hizo wamekuwa wakifanya doria kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi ambao ni ujirani mwema ambapo wamekuwa wakiweza kufichua wale wote ambao wanaingiza mifugo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria ambao wamekuwa wakipigwa faini huku wengine wakifikishwa mahakamani .



Kwa upande wake mkuu  wa hifadhi ya Mkomazi Donat Simon Mnyagatwa Alisema kuwa mbali na kuwepo na changamoto hiyo ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo alibainisha  kuwa  hili ni tatizo kubwa  linaloikabili hifadhi hiyo kwani maji ni uhai ,kuanzia kwa binadamu na hata kwa wanyama .

“Ni kweli ili nitatizo kubwa lakini pia tumeanza kuandaa mipango mathubuti  kwa ajili ya kutatua tatizo hili ambapo kwa upande wa binadamu tupo kwenye mkakati wa kuanza kuchimba visima virefu ili kuweza kupa maji mengi ambayo pia maji hayo yataweza kukusanywa kwa pamoja kwa ajili pia ya wanyama wetu,pia tunampango wa kuongeza mabwawa yaliyopo ndani ya hifadhi ili kuakikisha pia tunaondokana na changamoto hiyo”alisema Mnyagatwa



Aidha alibainisha kuwa mbali na changamoto hiyo pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundo mbinu ya barabara pamoja na nyumba za kuishi watumishi ambapo alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya familia tisa zinaishi ndani ya hifadhi  huku familia zingine zikiishi nje ya hifadhi ,pamoja changamoto hizo ameiomba Halmashauri ya same kupitia Tanroad kurekebisha barabara ya kuelekea hifadhini ili iweze kupitika kwa urahisi kwa kipindi chote.

Mnyagatwa alibainisha kuwa kwa lengo la ujirani mwema wananchi ambao wamekuwa wakizunguka hifadhi wamekuwa wakipatiwa mafunzo maalumu ya kutambua umuimu wa utunzaji wa hifadhi pamoja na kutambua mipaka ya hifadhi na athari za kuingiza wanyama hifadhini ,mathara ya uaribifu wa mazingira ambapo alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaelimisha na elimu hii imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhalifu ndani ya hifadhi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post