FILOMENA BENDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA NA VITONGOJI VYAKE USIKU WA VALENTINE DAY



Na Woinde Shizza,Arusha
Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina Filomena  music Band  ambayo makazi yake ni mkoani Kilimanjaro inatarajia kuwapagawisha wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake  ndani ya usiku wa wapendanao (valentine day).

Akizungumza na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa bendi hiyo Swaumu Kileo alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya kuitambulisha rasmi bendi hiyo kwa wakazi wa jiji la arusha pamoja na kuwapa  burudani ya nguvu wakazi wa jiji hilo ambapo  alibainisha kuwa burudani watakayo itoa itakuwa ya kihistori na aijawai kutokea.

Alisema kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kufanya show ndani ya jiji hili la Arusha kwa hivyo wanaimani wakazi wa jiji  hili na vitongoji vyake wataipokea kwa furaha na wataikubali kwakuwa hii ndio bendi ya kwanza kubwa iliopo  kanda ya  kaskazini.

"ujio huu wa filomena bendi utakuwa ni wakihistoria kwani kwanza ni bendi kutoka  mikoa hii hii ya kanda ya kaskazini pia ipo nyumbani kwaiyo ninaimani watafurahi na wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake wajitokeze kushuhudia bendi hii kwani hii ndio bendi yao ya nyumbani “alisema Swaumu
Aidha alibainisha kuwa katika siku hii ya valentine day  wameiandaa maalumu kwa ajili ya kuwaonyesha washabiki wao kuwa wanawajali hivyo watatumia siku hiyo kuwatambulisha washabiki wa mziki huu wa dance nyimbo za bendi hiyo   ambapo pia alisema watawaonyesha staili nyingi mpya ambazo azijachezwa na bendi zingine hapa nchini ikiwa ni pamoja  na kuonyesha jinsi kila mtu anavyotakiwa kutingisha yakwake.
Aidha alibainisha kuwa show hiyo itafanyika ndani ya ukumbi wa milestone garden uliopo jijini hapa huku akibainisha kuwa kwa upande wa viingilio V.I.P watalipa shilingi 20000 huku kawaida wakilipa shilingi 10000 kwa kila mmoja na kusema kuwa kwa wapenzi watakao pendeza kuliko wote wataondoka na bonge la zawadi .


kwa upande wa kiongozi wa bendi hiyo sety Mbeki alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya kila mtu atingishe yakwake   ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.

Alisema kuwa lengolao kubwa la kufanya onyesho hili ndani ya jiji la arusha ni pamoja kujitambulisha kwa wakazi wa la arusha na kuwaambia wasio wapweke tena kwani wamepata bendi mpya kutoka nyumbani kwao bendi ambayo ni yao  inatoka ndani ya kanda yao na ni watoto wa o.
Aliwasihi wakazi wa jiji la arusha na kanda ya kaskazini kwa ujumla kuwapokea kwa mikon o miwili na kuwapa ushirikiano ili waendelee kuwapa burudani zaidi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post