MSANII WA FILAMU ROSE NDAUKA NA MENEJA WAKE WAZINDUA JARIDA LITAKALOKUWA LIKITOKA KWA WIKI MARA MOJA

 Msanii wa Filamu nchini, Rose Ndauka (kushoto) na Meneja wake Ramaehan Mwanana wakionesha Jarida jipya litakalojulikana kama  Rozzie Magazine wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
 Meneja wa Ndauka Ramaehan Mwanana (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Rose Ndauka, akizungumza katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

MSANII wa filamu Tanzania, Rose Ndauka  amezindua jarida  jipya liitwayo Rozzie litakalotoka  mara moja kwa kila mwezi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi huo, Rose alisema dhumuni kubwa la jarida hilo ni kuelimisha, kuiburudisha, kuikosoa na kuichochea jamii katika kufikia malengo yao ya kimaisha  kwa ujumla  na kujenga taifa bora lenye maendeleo.

“Pia katika kurasa za ndani  za jarida hilo  zipo kurasa zilizobeba mambo ya fasheni, maisha pamoja na mambo mbalimbali yanayoikosoa jamii pale inapokosea,” alisema.

Alisema kuwa lengo la kutoa jarida hilo ni kuwafikia watanzania wote na nakala yake itapatikana  kwenye mtandao ya kijamii mara moja kwa kila wiki.

Alisema magazine hiyo anaitoa bure  kiwa watanzania wote  na litakuwa likitoa taarifa  taarifa mbalimbali  kwenye mitandao yote ya kijamii ambayo ni Facebook, Instagram, Twitter na You Tube.

Meneja  wa jarida la Rozzie, Ramadhani Mwanana, alisema wameanza kwa kuchapisha kopi 5,000 na jinsi wanavyoendelea waziongeza  nyingi zaidi.


Alisema jarida  hilo ltasambazwa katika mikoa yote hapa nchini  kwa kutumia magari makubwa ya mikoani, maduka mbalimbali pamoja na nyingine zitakazowezesha watanzania kupata magazine hiyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post