Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za (CCM) Mtoni
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akimkabidhi vifaa vya michezo Katibu Kata ya Mtoni kwa Azizi Ally vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke katika Hafla fupi ya kusheherekea miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika kesho Mkoani Singida ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu Dtk Jakaya Kikwete
Khamisi Mussa
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ametoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke.
Mtemvu alitoa vifaa hivyo ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kilele chake kitaifa kinafanyika leo mkoani Singida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mtemvu alisema lengo lake ni kuimarisha michezo kwenye kata hizo na kuwaepusha vijana kujiingiza katika vitendo vya kiovu na kujenga afya zao.