BREAKING NEWS

Wednesday, February 3, 2016

WAAJIRI WALALAMIKIA RUSHWA KUKWAMISHA BIASHARA

 Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka  akiwa anafafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha  waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha leo



 wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa  wakiwa wanajadili  kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua .

Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa  Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka  akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za  ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi 


Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.

Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.








Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates