BREAKING NEWS

Tuesday, March 8, 2011

BABU AZIDI KUTIBU WATU KWA KASI


mchungaji(babu)Ambilikile Mwasapile ambaye anatibu magonjwa mbalimbali akiwa anawapa watu maelezo kuhusiana na dawa hiyo ambayo mungu amemfunulia



hapa ni dawa hiyo ambayo inatibu magonjwa mbalimbali ambayo ni sungu ikiwa inachemshwa ili watu wakainywe



mti ambao babu anautumia kutibia watu mti huu unajulikana kwa jina la Mugariga ambao pia unatumika kutumia kama chakula cha twiga

Jeshi la polisi mkoani Arusha leo limewapeleka askari wilayani ngorongoro katika kata ya digodigo kijiji cha samange kwa mchungaji anayetoa dawa kwa ajli ya kuimarisha ulinzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Andengenye alisema kuwa jeshi la polisi limeamua kuongeza askari katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha amani na kuweza kusimamia eneo hilo.

Alibainisha nia ya haswa ya kuwapeleka polisi katika eneo hilo ni kusaidia kuangalia jinsi ya kuboresha huduma pamoja na jinsi ya kuharakisha safari watu wawewanaenda haraka na msafara unatembea .

Alisema kuwa mpaka kufikia jana kulikuwa na askari kutoka katika wilaya za karibu ambapo alisema kuwa kuna askari polisi kutoka loliondo na wengine kutoka katika wilaya ya Ngorongoro lakini kutokana na watu kuwa wengi wameamua kuongeza askari wengine kutoka mkoani ili kuweza kuimarisha amani.

"kulikuwa na askari pale lakini kwakuwa watu wameongezeka inabidi askari wetu waondoke Leo ili waweze kwenda kusaidi na kuimarisha ulinzi"alisema Andengenye.

Alibainisha kuwa kutokana na magari kuwa mengi wanawapeleka pia askari wa usalama barabarani ili ili kuweza kusaidia misafara ikaenda haraka sana.

Andengenye alisema kuwa kwa swala la kuzuia serekali hawazuii kwa maana ya kuzuia ila wanahamasisha watu wapunguze kwenda ili waliopo uko wapungue.

Alimalizia kwa kusema watu wanao enao enda wanatakiwa waamini kuwa wanatibika na wajitaidi kuwa wavumilivu wasubiri mpaka wenzao walioenda wapungue ili kuweza kusaidia mathara yasitokee na kusema kuwa wasiofie kwa sababu huduma bado ipo .

Mpaka sasa watu mbalimbali wanazidi kufurika kuelekea katika wilaya hiyo ya ngorongoro kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile (babu) ambaye ana toa tiba ya magonjwa mengi ambayo ni sungu na ambayo yametafutiwa dawa kwa muda mrefu lakini hayajapata dawa lakini yeye ndiye aliyebarikiwa na mungu na kupata dawa ya magonjwa hayo.

Mwandishi wa habari hizi alizungumza na watu mbalimbali ambao wameshaenda kunywa dawa hiyo na ambao bado hawajaenda kunywa nao walikuwa na mambo mbalimbali ya kusema mmoja wa watu hao alijitambulisha kwa jina la Roda peter ambaye yeye ni mkazi wa kijiji cha Samange naye alisema kuwa yeye anamshukuru mungu sana kwa kumletea mtu ambaye amepata dawa ya kutibu magonjwa haya sugu.

Yeye binafsi alisema kuwa alikuwa ameathiriki na virusi vya ukimwi likini mara baada ya kunywa dawa hii ya babu alienda kupima mara tatu na akikuta anavirusi kitu ambacho tangu apate hajawai kutegemea kama angekaa apate mtu wa namna hii ambaye atawatibu magonjwa mbalimbali.

"unajua nilivyokunywa hii dawa nilenda kupima mara ya kwanza baada ya siku saba nikakuta ninao ,nikaenda ya pili nikakuta ninao lakini nilivyoenda mara ya tatu uwezi amini nimekuta sina acha mungu aitwe mungu mbali na ilo siku amini nimepima zaidi ya hospitali tatu lakini nimekuta hamna acha tu kweli mtu anayemsema huyu babu vibaya alaaniwe kwani mimi kanitibu kabisa nilikuwa nimekata tamaa ya maisha"alisema Roda.

Kwa upande wa mtu mwingine ambaye yeye ajaenda ambay alijitambulisha kwa jina la Erasto Rafael alisema kuwayeye alikuwa haamini kama dawa hii ni ya kweli lakini kwa sasa ameanzakuamini kutokana na watu ambao anawajua kwenda na kuwaona wamerudi wakiwa tofauti na wengine wamepona kabisa.

"mimi nilikuwa siamini uezi amini ninabesti yangu alikuwa analazwa haongee anyi soda yani anafuata masharti ya dawa sukari lakini sasaivi anakunywa mbaya acha tu lazima ata miminiende."alisema rafaeli

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates