BREAKING NEWS

Thursday, March 24, 2011

YALIYOTOKEA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI YA WABUNGE WA KENYA NA TIMU YA WAZEE KLABU YA MKOANI ARUSHA


Rt.Hon AbdiRahin Abdi spika wa bunge la jumuiya ya afrika mashariki akiongea katika hafula fupi iliyoandaliwa mara baada ya mechi kumalizika



anayepatiana zawadi akiwa amevalia uniform nyeupe ni Mweshimiwa David. E. Ethuro na ndiye mwenyekiti wa klabu ya bunge la kenya ambao walikuja jijini hapa kushiriki mechi baina yao na wazee klabu.



Warembo pia walikuwepo wakipata kinywaji mdogomdogo



Apo mwenyekiti wa timu ya klabu ya wazee ya mkoani Arusha Danford Mpumilwa aliyevaa suti nyeusi akifuatilia mpira wakati timu yao ilivyokuwa ikicheza huku spiker wa bunge la jumuiya akipewa maelekezo na mmoja wa wachezaji wa timu ya wazee klabu


Apo wabunge na wazee klabu wakiendelea kusherekea



Huyo mrefu aliyevalia shati jeupe ni spiker wa bunge la Afrika mashariki ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi apo akiendelea kufurahia mechi ambapo alisema mechi hiyo ni mojawapo ya maana ya jumuiya hiyo

TIMU ya mpira wa miguu ya wabunge kutoka nchini Kenya mwishoni mwa wiki walipigwa kipigo cha bao 4-3 ya ugenini katika mechi ambayo walikuwaja kucheza na klabu ya Wazee ya mjini hapa.

Mchezo huo wa kukata na shoka ulipigwa jumamosi katika uwanja wa mpira wa General Tyre uliopo Njiro nje kidogo ya mji ya Arusha.

katika mechi hiyo timu ya wabunge wa kenya ilionyesha kulimewa sana katika kipindi cha kwanza na kuweza kuweza kuwapa nafasi wenyeji wao ambao ni wazee Klabu ambao waliweza kujidumbukizia magoli nyavuni kama mvua.

timu hii ya Wazee ya jijini hapa iliweza kujiandikia goli la kwanza kunako dakika ya 12 ya mchezo kupitia kwa mchezaji wao Wyclif ketto huku goli la pili wakilipatakupitia kwa mchezaji wao Sherkh Abu ambaye alipicha shuti kali ambalo liliwaacha wachezaji wa timu ya wabunge wa kenya wakiduwaa goli ambalo lilifugwa kunako dakika ya 16.


Timuy ya wazee iliweza kujiongezea goli lingine la tatu kupitia kwa mchezaji wao Ibrahimu Jamali ambaye aliliweka kimnyani kunako dakika ya 21 dakika tatu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika timu ya wazee iliwekuongeza goli lingine ambapo walilipata kupitia kwa mchezaji wao Sherkh Abuu ambalo goli hilo lilisababisha hadi kipindi cha kwanza kumalizika timu hii kuwa na magoli manne huku timu ya bunge fc ya kenya ikitoka kapa.

waliporudi kipindi cha pili timu ya Bunge Fc ya kenya kuonyesha mabadiliko kwani mara tu baada ya kuingia waliweza kuonyesha kasi kubwa na ilipotimu kunako dakika ya 65 ya mchezo Mchezaji Elija Echwara aliweza kuipatia timu yake goli la kwanza goli ambalo liliwafanya mashabiki wa timu hiyo ya bunge la kenya kusimama wote na kushangilia.

kenya waliweza kupata nguvu zaidi huku timu ya wazee klabu ikionekana kulemewa na kuzidiwa nguvu na kuwapa nafasi ya kuendelea kufunga timu ya Bunge Fc na ilipotimu dakika ya 76 Antoni Mnene aliweza kuipatia timu yake goli la pili ambapo kenya walianza mpira tena na baada ya dakika moja waliweza kuongeza goli la tatu goli ambalo lilisababisha hadi kipenga kulia matokeo yalikuwa wazee klabu wakiongoza kwa magoli manne huku Bunge FC wakiwa na magoli matatu.



Nilizungumza na kocha wa timu ya bunge Fc ya kenya Naman Agengo naye alisema kuwa nia ya kuja kucheza mechi na timu hii ya wazee ni kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kupitia michezo.

Alisema kuwa wamefurahia mechi ambayo wamecheza na pia mechi hiyo imekuwa kiburudisho kwao kwani wamecheza wamefugwa lakini ndo mchezo.

Alisema kuwa michezo ni umoja michezo ni nguvu na pia michezo ni afya alisema kuwa wakiwa pamoja jumuiya ya afrika mashariki pamoja watatekeleza lengo lao la nchi zote za afrika mashariki kuungana.'

"lengo letu ni kushiriki mchezo katika nchi hizi zetu za afrika mashariki na michezo itatuunganisha nchi zetu zikiungana basi nchi na kutimiza lengo la kumuungana wa nchi tano"alisema Agengo


kwa upande wa mwenyekiti wa klabu hiyo,Danford Mpumililwa alisema kuwa mechi ilikuwa nzuri matokeo ni mazuri na wao wataendelea kushirikiana na nchi hizi katika michezo lengo ikiwa ni kujenga ujirani mwena.

Alisema kuwa pia wanampango wakenda nchini kenya kushiriki mechi na sio kenya tu bali watahakikisha wao kama wazee klabu wanaenda kucheza mechi mbalimbali katika nchi mbalimbalimbali.



Klabu ya wazee ya mkoani Arusha ni mojawapo ya klabu ina jumla ya wanachama 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambao hufanya kazi mkoani hapa katika nyanja za kitaifa na kimataifa.
sy

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates