Thursday, March 24, 2011
MAKAMU WA RAISI ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA BIOGES
Posted by woinde on Thursday, March 24, 2011 in | Comments : 0
MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho kutwa,machi 26 mwaka huu katika hafla ya uzinduzi wa programu ya Bioges kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini CAMARTEC kilichopo Njiro mjini Arusha.
Mkurugenzi mkuu wa Camartec Eng. Evarist Ng'wandu alisema kuwa makamu wa Rais kabla ya kuzindua Frogramu hiyo anatembelea shamba la mkulima mmoja wa kijiji cha Moivo Seleman Ally kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa kwa kutumia biogas.
Alisema kuwa,katika shamba la mkulima huyo wataweza kujifunza mambo mengi jinsi ambavyo teknolojia hiyo ya biogas inavyosaidia katika shughuli nyingi za kilimo na nishati,hivyo kuwawezesha watu wengi kuondoakana na gharama kubwa za kutegemea nichati ya umeme wa tanesco pekee .
Ng'wandu alifafanua zaidi kuwa, baada ya kujionea mfano wa matumizi ya teknolojia ya Biogas kwa mkulima huyo makamu wa Rais ataendelekea moja kwa moja katika Kituo hicho kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa programu hiyo biogas .
Alisema kuwa, teknolojia hiyo ilikuwepo tangu mwaka 1970 ispokuwa uzinduzi rasmi ulikuwa bado haujafanyika , hivyo asilimia kubwa ya wananchi kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wameweza kunufaika na teknolojia hiyo kwa ukaribu zaidi baada ya kuizindua rasmi.
Alisema Kituo hicho hadi sasa kimefanikiwa kutoa elimu ya matumizi ya teknolojia hiyo kwa jumla ya watu 490 kutoka mikoa ya Arusha, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Mnyara , na Singida.
Ambapo watu hao wamefundishwa kuhusiana na umuhimu wa kutumia teknolojia hiyo kupitia programu ya Uenezi wa Biogas ngazi ya Kaya huku msimamizi wake akiwa ni Camartec.
Ng'wandu aliwataka wananchi walio wengi kutoka mikoa mbalimbali ambao hawajanufaika na teknolojia hii kujitokeza kwa wingi kwani ni nafuu na haina gharama yoyote kutoka na kuwa utengenezaji wake unatokana na mchanganyiko wa vitu vilivyochachuka kama kinyesi na mimea.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia