MBUNGE wa jimbo la Arusha,Godbless Lema amejitolea kusafirisha watu 100 wenye magonjwa sugu ambao ni wakazi wa jimbo hilo kwa lengo la kwenda kupatiwa matibabu kwa mchungaji,Ambilikile Mwasapile aliyepo katika kijiji cha Samunge Loliondo mkoani Arusha.
Lema amefikia hatua hiyo baada ya kuguswa na idadi kubwa ya wananchi wa jimbo hilo wenye matatizo mbalimbali ya magonjwa sugu ambao wameshindwa kusafiri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Kadhalika mbunge huyo ameamua kukata nusu ya fedha kiasi cha sh,50 milioni kati ya sh,90 milioni alizopewa na bunge la jamhuri kwa lengo la kujinunulia gari, ili fedha hizo zitumike kuwasaidia wakinamama kwa kuanzisha mfuko maalumu wa kukopeshana.
Akizungumza na mamia ya wakazi wa jimbo hilo ambao walifika kujiandikisha kwa ajili ya safari ya kuelekea Loliondo , nje ya ofisi ya mbunge huyo,Lema alisema kuwa binafsi ameamua kujitolea fedha za kuwasafarisha watu 100 kwa sasa, ili wakapatiwe matibabu kwa mchungaji Mwasapile.
Hata hivyo Lema,alitumia fulsa hiyo kuwasihi na wabunge wenzake waige mfano huo kwa kuwajali wenye shida japo kwa kiasi kidogo kwa kujitolea.
Alisema kuwa ameguswa na afya za wakazi wa jimbo la Arusha na kuamua kuingia gharama za kuwasafirisha kwa awamu ya kwanza lakini zoezi hilo litakuwa endelevu kadri ya siku zinavyokwenda na idadi yao itakavyokuwa ikiongezeka.
Aidha aliwataka wakazi wengine wa Arusha wenye uwezo kifedha kujitolea kuwasafirisha wagonjwa mbalimbali huku akiwataka kuguswa katika kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kupatiwa matibabu.
Akizungumzia suala la kujitolea kwa kukata sehemu ya fedha alizopewa na bunge, alisema kuwa ameamua kukata sehemu ya fedha kiasi cha sh,90 milioni aliopewa na bunge ili fedha hizo awarudishie wananchi kama sehemu ya mchango wake wa kuhakikisha kuwa akinamama wanajiletea maendeleo kwa kutumia fedha hizo kwa kukopeshana.
Hatahivyo,alisisitiza kuwa yeye kama mbunge wa Arusha haoni haja ya kuwa na gari la kifahari ihali wananachi wake wakiteseka na kudai yuko tayari hata kutembea kwa mguu kuliko kuwa na gari hilo la kifahari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia