Bodi ya usajili wawandisi nchini ERB, imewataka wahandisi kutumia taaluma yao vizuri ili ,kujengea sekta ya waandisi heshima.
Hayo yameelezwa mjini Arusha na mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Niratubu Lema ,wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja wa mashauriano na waandisi uliowashirikisha wakuu wa vijana waandisi wa mikoa ya kilimanjaro,Tanga na Arusha.
Profesa Lema alisema kuwa pamekuwepo na matukio kadhaa kwa baadhi ya waandisi kukiuka taaluma nakanununi za kiutendaji wahandisi hali inayovunja heshima yataaluma hiyo.
Alisema kuwa kwa upande wa changamato ambazo wanazoni pamoja na kukosa sehemu ya kufanyia kazi za vitendo kitu ambacho bodi imeweka utaratibu na mkakati wa kuwezesha vijana amao wanamaliza shule ya uandisi waweze kufanya kazi za vitendo na kusajiliwa.
Alisema kuwa mpaka sasa waandishi waliosajiliwa ni waandisi 9000 na katika hao wanawake ni 500 kitu ambacho kwa upande wa wanawake idadi hairithishi kabisa.
"kwa sasa tunataka tujitaidi waandisi wa kike waongezeke kwani ni wachache sana tunania ya kuwa na waandisi wanawake wanaolingana na wanaume iwapo wasipo lingana basi angalau wafikie ata nusu ya wanaume"alisema Lema
Naye mwakilishi ubalozi wa serekali ya Norway inayofadhilimkutao huo Bibi Malin Liyet ameitaka ERB kuendeleza kozi zake inazotoa kwa wahandisi wa kike,ili kuweka uwiano sawa kati ya wahandisi wa kike na wakiume.
Alisema pamoja na kuwepo wahandisi wa kike, idadi yao ni ndogo hali inayosababishwa na mazingira yasiyovutia kwa wanawake ktika kusomea masomo ya kiuhandisi.
Bibi Luyet alisema katika nchi ya china uchumi wao umekuwa kwa kiwango kikubwa hali iliyochangiwa kwa wanawake wa nchi hiyo kujiingiza kwa wingi katika sekta binafsi ikiwemo ya Uhandisi.
kwa upande wake mwandisi wa kike aliyebobea katika fani hii Magret Mnyage alisema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zimewafanya wanashindwa kuwa na waandisi wengi wa kike ambapo alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakiogapa kwenda kusomea masomo haya kutokana na masomo kuwa magumu.
"unajua watoto wetu wa kike wamekuwa wakikatishwa tamaa na kudaiwa kuwa masomo ni magumu kitu ambacho sio cha kweli hivyo sisi kama wazazi kwanza tunatakiwa kutowaoposha watoto bali tuwahamasishe waende wakasome masomo ya sayansi na physicics ili wakitoka huko waweze kusomea fani hii kwani wakizidi kuogopa ndipo tutazidi kukosa waandisi wa kike"alisema Mugage.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia