Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya ngorongoro kata ya digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine wakilazimika kupoteza maisha kutokana na msongamano wa watu na kuchelewa kupata huduma.
Wananchi hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kujijihicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa muda mrefu na ambayo walikuwa hawategemei kama wangekaa wapate dawa zake.
Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji Mwasapile huku wengine waliofika katika nyumba ya mchungaji huyo na kupata huduma wakiwa wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri mara baada ya magari ambayo yaliwaleta kuondoka kutokana na kukaa muda mrefu.
Mbali na kuacha na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu wengi wao wamekuwa wakipata shida sana kwa ajili ya malazi na chakula kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu wanao wakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda hata wa siku tano na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata chakula kwa njia ya shida sana hali ambayo inaleta hofu kubwa kwani watu wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kuotokana na msongamano huo wawatu wengi .
Pia katika msongamano huo wawatu umeleata mathara kwani pia kunabaadhi ya wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu watu saba walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.
Mwandishi wa habari hizi aliweza kushuhudia maiti hizo ambapo mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine wakiwa hawajiwezi kabaisa.
Pamoja ya kuwa mchungaji Mwasapile alijitaidi sana kuhudumia wagonjwa ambao walifika sehemu hile lakini haikusaidia nahadi kufika jana jioni ilibidi waongeze wachungaji wengine wawili kumsaidi mchungaji huyu ili kuweza kupunguza watu kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wagonjwa wanazidi kumiminika zaidi .
Mchungaji Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu watu bado wanaongezeka na wanatoka katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali hali ambayo itafikia mahali hata itamgarimu mtu kuchukua hata waki tano kupata huduma.
Mchungaji huyo alisema kuwa yeye mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi tu na ilipofika mwaka jana mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.
“na mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu na kweli alikuja mama mmoja wa hapa hawa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza na watu wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile
Alisema kuwa dawa hii ainyeki mara mbili tiba yake ni mara moja tu na alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa HIV itanawatibu baada ya siku 21 ambapo alifafanunua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande wawatu waenye kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo dawa tu.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena, Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Kwa upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wengeji ambapo alifafanua kuwa awali wenyeji walikuwa wanazarahu dawa hiyo na kusema kuwa hawamuamini lakini baada ya kuona wageni wengi wanajitokeaa kunda kunywa ndio na wao wameanza kujitokeza kwa wingi.
Pia alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa waho kujitaidi kuwaleta wagonjwa wakiwa angalau wananafuu kwa kiasi na wasiwachukuwe wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa ivi msongamano wawatu umezidi hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumia .
”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiw amahutiti kwani ndo inaweza kuwasababishia mathara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kuupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambaozo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
Pia gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa wakiwa wanauza shilingi 2000.
Alisema kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipata kila siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maramu Juma alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifaika ngorongoro akiwa anaumwa na amebebwa lakini tangu anywe iyo dawa amesisimama mwenyewe na anatembea kitu ambacho amemshukuru mungu kwa kumleta mtumishi huyu katika nchi ya Tanzania.
Mbali na wagonjwa ambao walihudhuria katika kujiji hicho waliomba jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza gasia ambao wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili kuweza kusaidia vurugu zisitokee.
Walisema kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.
“tunaomba jeshi la polisi liongeze idadi ya askari waweze kusimamia utaratibu kwani muda mungine babu anashindwa fanya kazi kutokana na vurugu unakuta mtu amekuja hapa leo na kuna mungine kaja juzi yule wa leo ataki kufuata utaratibu uliowekwa analeta fujo kitu ambacho kinaleta ata uvunjifu wa amani “alisema mmoja wawagonjwa aliyejulikana kwa jina la Godfrey Lymo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia