Thursday, March 24, 2011
ZINDUKA WOMEN CENTER
Posted by woinde on Thursday, March 24, 2011 in | Comments : 0
Wanachama wa kikundi cha zinduka wakimuombea mbunge wajimbo la Arusha mjini alipofika kuwawezesha
KITUO cha Zinduka Women Centre kilichopo Njiro mkoani Arusha kimefanikiwa kuunda jumla ya vikundi vidogovidogo 27 vya uwekaji wa kiba kwa lengo la uzalishaji mali na kuwakopesha wanawake wa kikundi hicho.
Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na mkurugenzi wa kikundi hicho,Sister Mary Rashmi wakati akisoma taarifa ya shughuli ya za miradi mbalimbali ya mwaka 2010 hadi 20111 katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika kituo hicho.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kituo hchao kimefanikwia kupiga hatua katika kuwajengea uwezo wanawake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuendesha miradi ya mara kwa mara sanjari na kupanga,kutathmini mchakato wa kuwawezeha.
Hatahivyo,alisema kuwa katika mfumo wa benki za jamii vijijini(Vicoba) kituo chao kimefanikiwa kuunda vikundi vitano vya wnawake 30 kila kimoja ambapo wka sasa vinatekeleza majukumu yak echini ya mwalimu Oliver Mollel kutoka shirika la Pathfinder Interenational.
Sister Rashmi alisisitiza kwa kueleza kuwa kituo cha Zinduka pia kimefanikiwa kutoa elimu ya chekechea kwa watoto wadogo 90 katika kijiji cha Loiborsidebt wilayani Simanjiro mkoani Manyara wanaosoma chini ya mti.
Awali akisoma risala yake mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema aliwataka wanawake katika kikundi hicho kuutumia muda wao mwingi kuzungumzia masula ya manedeleo na kuachana na majungu.
Lema aliwambia kuwa vitendo vya kusengenyana na kupigana vijembe kamwe havitawasaidia huku akidai kukipatia kipaumbelea kikundi cha Zinduka katika kuwapatia mikopo ya riba nafuu kupitia kiasi cha sh,50 milioni alichokitoa kwa lengo la kuwasaidia mikopo wakinamama wakazi wa jimbo la Arusha mjini.
“Muda wenu utumieni kuzungumzia maendeleo ,eti Fulani amevaa nguo Fulani hiyo inakuhusu nini si yak wake,acheni majungu na kusengenyena’alisema Lema
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia