Kikosi cha timu ya simba ambacho kitaenda kinatarajia kuondoka jumamosi kwenda nchini kongo kukabiliana na timu ya Tp Mazembe kinatarajiwa kutajwa kwesho jijini Dar es salaam.
Akizungumza na lebeneke hili meneja wa timu ya simba Inocenti Njovu alisema kuwa kikosi rasmi kitatangazwa kesho ambacho kitakuwa na wachezaji 20 huku benchi la ufundi likiwa na viongozi watano ambao wataenda.
Alisema kuwa mpaka sasa hamna mchezaji ata mmoja ambaye ni majeruhi na wanatarajia kurudi na ushindi huko waendapo kwani mazoezi waliyoyafanya ni mazuri na haliya hewa ambayo wamefanyia mazoezi ni sawa na ya kongo.
"unajua kitu kingine kinachonifanya nijiamini ambacho ndo kilikuwa labda kinanitatiza ni hali ya hewa tulijua hali yahewa inaweza kutuletea shida kwani kule kuna baridi na dar joto sasa ingewaletea wachezaji shida ila kwa apa arusha tulivyokuja kucheza tukaona hali ya hewa inaelekea kuendana na kule tumeamua kukaa apa ivyo wachezaji wamezoea hali ya hea na hawatapata tabu"alisema Njovu.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa mechi ni ngumu lakini ushindi ni lazima kwani wamejiandaa vizuri na mazoezi akisisitiza kuwa mchezo ni maandalizi .
"unajua mchezo ni maandalizi sasa wewe unakaa tu bila kufanya zoezi unasubiri ukicheza ufunge si ndoto izo sisi tumejiandaa tumefanya zoezi ivyo tunauhakika wa kushinda "alisema Njovu.
Timu hii ya simba ambayo ilikuja jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita na ikakutana na timu ya AFC na kuifunga magoli 2-0 na mara baada ya mechi waliamua kuweka kambi ya siku tatu jijini hapa ambapo walikuwa wakifanyia mazoezi katika uwanja wa kendauni imeondoka jijini hapa leo kuelekea dar kwa ajili ya maandalizi ya safari yao ya kenda nchini kongo.
wakati huo huo Vingozi wa timu ya AFC ya jijini Arusha ambayo inashiriki ligi kuu na ndio timu pekee inayoshikilia mkia wamebainika kuwa ndio chanzo cha kuifanya timu hiyo kushindwa kufanya vyema katika ligi.
Hayo yalisemwa na kocha msaidizi wa timu ya Simba Amri Saidi wakati alipokuwa akiongea na blog hili jijini hapa.
Alisema kuwa anawatupia lawama viongozi wa timu ya AFC kwa sababu wao ndio walioshindwa kufanya maandalizi mapema na kusabaisha timu hiyo kuwepo hapo ilipo kwa sasa.
Alibinisha kuwa wakati wa maandalizi ambapo timu ilitakiwa iwepo kambini timu haikuwepo kambini na badala yake viongozi wakawa wanarushiana maneno ya fitina tu.
''kipindi timu nyingine zipo kwenye maandalizi timu hii ya AFC haikuwa kambini kulingana na maneno maneno na majungu ya viongozi badala wakae waamue kupeleka timu kambini wakajiandae wao wanapigiana majungu tu kweli kwa hali hiyo timu ikishuka daraja watalalamika"alisema saidi\
Alisema kuwa siri ya ushindi ni kuandaa timu mapema kwakuwaweka kambini kwa pamoja na wafanye zoezi sasa viongozi wao walikaa wanalumbana ligi imeanza wao ndo wanaita timu hapo lazima wangeshuka tu .
''sasa ujaweka timu kambini ukifungwa ata magoli hamsini utalalamika waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi sasa wao wamekuja kugutuka mwishoni wao wakubali matokeo tu bwana "alisema.
Sisi kama simba tulikaa kambini kambini mapema kuandaa timu na tunafanya mazoezi kila siku sasa kweli unategemea mimi nimefanya mazoezi wewe ujafanya unategemea utanifunga kwaiyo mimi lawama zangu nawatupia viongozi mana ndo chanzo cha yote haya.
Alisema kuwa kwa mwaka huu katika ligi kuu mara baada ya ligi hii kuisha hawataki timu ambazo ni malagalasa kwa iyo timu zote ambazo zimepanda zijiandae vyema akiwatolea taathari timu ya Coast Union ya jijini Tanga ambayo nayo imepita.
"kwenye ligi ijayo hatutaki timu malagalasa tunataka timu ngangari ili ligi iweze kuwa na ushindani wa kutosha kama nyie ni magalasa jikataeni mapema sisi timu za kufugwa fugwa hatutaki tunataka mpira Tanzania upande "alisema Saidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia