BREAKING NEWS

Thursday, March 24, 2011

DIWANI APINGA KUFUNGWA KWA BARABARA,AAMURU IFUNGULIWE HARAKA

KATIKA hali isiyo ya kawaida diwani wa kata ya Kaloleni wilayani Arusha kupitia
Chadema,Charles Mpanda maarufu kama rasta juzi amefanya ziara ya kushtukiza
katika kampuni ya ujenzi ya Group Six International Limited iliyopo katika eneo
la Florida kwa lengo la kutaka kujua sababu za kampuni hiyo kufunga mojawapo ya
barabara ndani ya kata yake.

Barabara hiyo ni ile itokayo katika eneo la mzunguko wa Florida hadi ofisi ya
kata ambapo ilifungwa na kampuni hiyo mnamo machi 11 na kutarajiwa kufunguliwa
Aprili 10 mwaka huu kutokana na kampuni hiyo kutekeleza zoezi la ujenzi katika
eneo hilo.

Diwani huyo alifanya ziara hiyo hivi karibuni majira ya saa 12.10 jioni akiambatana na
madiwani wenzake wa Chadema ambapo mara baada ya kuwasili katika eneo hilo
alikutana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwemo raia wa kichina na
kasha kutaka maelezo ya kina ya kufungwa kwa barabara hiyo huku akitoa masaa
machache kufunguliwa barabara hiyo.

Kabla ya kutaka ufafanuzi wa kufungwa kwa barabara hiyo,Mpanda alisema kuwa
kitendo cha kufungwa kwa barabara hiyo kumepelekea kero na usumbufu kwa wakazi
wa kata ya Kaloleni wanaokwenda katika kituo cha polisi cha kata hiyo sanjari na
kituo cha afya cha Kaloleni kupatiwa huduma sanjari na wakazi wa jirani na
maeneo hayo kuzunguka umbali mrefu.

‘Ninaomba maelezo ya kina kwanini mmefunga hii barabara wakati wananachi wangu
wanalalamikia kupata kero kutokana na zoezi hili,embu nipeni maelezo ya kina
kwanini mmeifunga”alisikia Mpanda

Mara baada ya swali hilo ndipo alipojitokeza mfanyakazi wa kampuni hiyo
aliyejitambulisha kuwa ni meneja utawala aitwaye,Julius Macha na ndipo
alipomwleleza diwani huyo ya kuwa wameifunga barabara hiyo kutokana na
kutekeleza ujenzi katika eneo hilo kwa baraka za uongozi wa manispaa ya Arusha.

Huku akimwoyesha barua yenye kibali cha kuifunga barabara hiyo yenye
Kumb.AMC/ME/119/VOL.1V/66 ya desemba 22 mwaka jana na kusainiwa na
Injinia,Fordia Mwankenja meneja huyo alimweleza kuwa wao walifuata taratibu
zote.

Meneja huyo alidai kuwa katika kutekeleza taratibu hizo pia wanalipia kiasi cha
jumla y ash,300,000 kwa siku kama gharama za kuifungwa barabara hiyokwa uongozi
wa manispaa ya Arusha hatahivyo walipoombwa mifano ya risiti za malipo na diwani
huyo waligoma kuzitoa.

“Mheshimiwa sisi tumefuata taratibu zote za kuifunga barabara hii barua hii hapa
na tena huwa tunalipia laki tatu kwa siku kamam gharama za kuifunga hivyo sisi
hatuna makosa kabisa”alisema Macha

Mara baada ya majibu hayo diwani huyo alionyesha kutoridhishwa nayo na ndipo
akautaka uongozi wa manispaa ya Arusha kutoa maelezo ndani ya masaa 12 kuhusu
kufungwa kwa barabara hiyo kabla ya kuchukua hatua kali za kisheria.



Kufuatia sakata hilo gazeti hili lilimtafuta mkurugenzi wa manispaa ya
Arusha,Estomi Chang”a kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini bila mafaniko
kwani iliita muda mrefu bila kupokelewa lakini alipotafutwa injinia aliyetia
sahihi ya kuidhinisha kibali hicho aliyetambulika kwa jina la Fordia Mwankenja
alikataaa kuzungumzia suala hilo kwa madai yeye si msemaji.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates