Thursday, March 24, 2011
MCHUNGAJI AWAKUSANYA WENGI KUWAPA DAWA
Posted by woinde on Thursday, March 24, 2011 in | Comments : 0
waheshimiwa nao wapo kwa babu bwana usipime
Jeshi la polisi mkoani Arusha limeendelea kuimarisha ulinzi kwa mchungaji mstaafu Ambikile Mwasapile anaetoa dawa katika kijiji cha Samnge kilichopo ndani ya wilaya ya Ngorongoro maarufu kwa jina la Babu kufuatia tuhuma zinazosemekana kuna baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kupanga mbinu za kuiba fedha zake.
Akiongea na gazeti hili kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha alisema kuwa wao kama jeshi la polisi bado hawajapata taarifa izo rasmi ila wameimarisha ulinzi zaidi ili kitendo kama hicho kisitokee.
Alisema kuwa mbali na hilo kwakuwa wameweza kuzipata watahakikisha fedha za babu huyo azikaii hapo ili kuweza kumueka babu huyo katika ali ya usalama zaidi na pia kutakuwa na watu wanamlinda babu huyo ili kuweza kumnusuru na watu ambao wamepanga kumfanyia mabaya.
Taarifa za awali ambazo zililifikia gazeti hili zilisema kuwa kunabaadhi ya watu ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi wamepanga njama za kumvamia babu na kuchukuwa fedha hizo.
zilisema kuwa babu huyo amekusanya ela nyingi sana ambazo ni shilingi mia tano tano hiyo wanapanga njama za kumfuaata na kuzichukuwa.
Mbali na hilo wafanya biashara wa nyumba za kulala wageni mkoani hapa wamekuwa wakifurahia huduma ya babu na kusema bora iendelee kulingana na kupata wateja wengi zaidi hali hiliyosababisha wao kupandisha bei za malazi.
Wakiongea na gazeti hili wafanya biashara hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa kumekuwepo na wingi wawageni ambao wanakuja kulala mkoani hapa hivyo imewalazimu wao kupandisha bei ili kuweza kupata faidia zaidi.
akizungumzia swala hilo mfanya biashara mmoja wapo aliyejulikana kwa jina la Jackline Mushi alisema kuwa wao wamefurahia sana kwani biashara inatembea hali ambayo ilikuwa awali haitembei.
"unajua mwanzo kabla babu ajatokea biashara ilikuwa haiendi kwani tulikuwa tunakaa ata siku tatu atujajaza lakini sasa ivi tunajaza sana kwani tumefikia hatua hadi tumepandisha bei za vyumba unakuta chumba cha shilingi elfu 25000 tunatoa hata kwa shilingi elfu 30000"alisema Mushi.
nilizungumza pia na mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawalali naye alisema kuwa watu wanazidi kuongezeka kila siku na kwa sasa foleni ipo mpaka porini hali inayosababisha watu ambao wapo nyuma kukosa uduma za kijamii.
Alisema kuwa tatizo la wananchi wamekuwa sio waelewa kwani wanaambiwa wasiende mpaka foleni ipungue lakini hawasiki ali ambayo inasababisha wakienda huku kupata shida na kuteseka sana.
"unajua foleni iko mbali ipo porini mno yaani ata uko walipo ata huduma ya chakula hamna watu wanateseka sana jamani wananchi wasikie wasiende bwana"alisema Wawalali.
Kwa upande wa mvua alisema kuwa kwa sasa mvua imepungua na magari yanapita ila kuna baadhi ya magari ambayo yameshidwa kupita kutokana na tope ambalo lipo pia alibainisha kuwa ile mito ambayo ilikuwa imefurika mpaka inashindwa kupitisha magari kwa sasa imepungua hamna mvua tena.
Alisema kuwa kwa sasa folini nindefu na kunamagari zaidi ya elfu tano huku akibainisha kuwa pia watu walioenda kunywa dawa ni zaidi ya elfu 40.
Alitoa wito kwa wananchi ambao wapo njiani wanaelekea kwa babu kuwa wasubiri kwanza mpaka watu wapungue ndio waende ili kuweza kuepuka na usumbufu pamoja na mateso.
"watu wanaokuja jamani wasubiri kwanini awataki sikia vitu ambavyo wanaambiwa na serekali unajua wao wanakuwa wabishi ila uku ni foleni vibaya na foleni ilipofika kwa sasa hamna chakula wala huduma yeyote ivyo watateseka sana "Alisema Wawalali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia