Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha,
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza maelezo ya namna ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha Unyunyuziaji wa Viuatilifu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, 2017. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Kushoto) akitembelea baadhi ya maeneo ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitumia mashine ya Kunyunyizia viuatilifu wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini maelezo ya namna maabara ya kupima masalia ya Viuatilifu inavyofanya kazi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha
Watumishi wa serikali wanaofanya kazi katika Taasisi ya Utafiti
wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical
Pesticides Research Institute-TPRI) wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi
kwa Weledi, Bidii na Nidhamu.
Kauli hiyo imetolewa Leo 16 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa
Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na
Vitengo wa Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha.
Mhe Mwanjelwa aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii,
Juhudi, Maarifa na Ubunifu kwani kufanya hivyo kutathibitisha matokeo chanya
katika utendaji wao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa moyo na uvumilivu
mkubwa pamoja na kuwepo kwa kadhia ya upungufu wa watumishi.
Sambamba na Taasisi hiyo kuwa na jukumu la kufanya utafiti,
kutoa huduma za usajili na udhibiti wa viuatilifu, Mafunzo kuhusu visumbufu na
kufanya hifadhi ya Bioanwai husika ili kuchangia uhakika wa chakula lakini pia
ina jukumu la kuendelea na kudumisha mashamba darasa kwa ajili ya Utafiti na
mafunzo kwa wadau hususani katika matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu.
Aidha, Alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret
Mollel kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kusimamia Taasisi hiyo ikiwa ni
pamoja na umakini wa Taasisi katika kufanya kazi zake katika kipindi cha miaka
10 ya utekelezaji wa muundo mkakati wa TPRI (2005-2015).
Alimsihi Mkurugenzi huyo anayesimamia Taasisi hiyo ya (TPRI)
iliyotungiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The TPRI Act
No 18 of 1979) ikisimamiwa na Wizara ya Kilimo, kuongeza ufanisi zaidi katika
usimamizi wa kazi kwa mujibu wa sheria na Taratibu za nchi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia