Saudi Arabia imelaani hatua ya
Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel huku pia shutuma
zikizidi kuongezeka kufuatia hatua hiyo.
Katika taarifa, taifa hilo la ghuba lilisema kuwa tangazo hilo la Trump sio la haki.
Lakini waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alilitaja tangazo hilo kuwa la kihistoria.
Hatua hiyo ya Ttrump ilibadilisha sera za miongo kadha za Marekani.
Hatma ya mji wa Jerusalem ni moja masuala makuu kwenye mzozo katika ya Israel na Palestina.

Mataifa 8 kati ya 15 ambayo kwa sasa ni wanachama
wa baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa yametaka shirika hilo kufanya
mkutano wa dharura kufuatia uamuzi huo wa Marekani.
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni jambo ambalo halijatambuliwa kimataifa na hadi sasa nchi zote zimeweka balozi zao kweny mji wa Tel Aviv.
Jerusalem una semue takatifu kwa dini tatu za kiyahudi, kiislamu na kikristo.

0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia