NGORONGORO WAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI
Posted by
woinde
on
Monday, December 18, 2017
in
Habari
MATUKIO
|
- Wanaharakati
wa kupinga ukeketaji wakisikiliza kwa makini mafunzo kabla ya kuanza
kampeni ya mwezi mmoja ya kupinga ukeketaji wilayani Ngorongoro. Mafunzo
hayo yaliratibiwa na Shrika la UNESCO. Kampeni hiyo inafanywa kwa
ushirikiano wa UNESCO, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Baraza la
Wazee wa Mila wa Kimaasai (Laigwanan). Kampeni hiyo imeanza Tarehe
5/12/2017 na itaendelea kwa mwezi mzima.
- Afisa
wa UNESCO anayewakilisha miradi ya Ololoswakan Wilayani Ngorongoro
Bwana Hamidun Kweka akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Oloirien
wilayani Ngorongoro madhara ya ukeketaji katika uzinduzi wa kampeni ya
kupinga ukeketaji wilayani humo. Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Tarehe
5 na zitadumu kwa mwezi mmoja.
- Ngariba
mstaafu akiimba na watoto nyimbo za kupinga ukeketaji baada ya mafunzo
ya kuwaelimisha madhara ya ukeketaji katika shule ya msingi Oloirine
wilayani Ngorongoro mnamo Tarehe 7, 2017.
- Wafanyakazi
wa UNESCO na Walimu wa Shule ya Msingi Oloirien wakiwa pamoja baada ya
uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukeketaji wilayani Ngorongoro.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia