Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Royal Soap, Jackline Mbaga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Star Oil Tanzania Limited , Ester Dotto, Meneja Mkuu wa Mo Assurance Limited, Kura Bonniface, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji, Meneja Mauzo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Holding Limited, David Mziray, Ofisa wa kitengo cha Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Jessica Julius, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Textiles, Godfrey Ndimbo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Food and Packaging, Anna Zongo wakiwa na tuzo nne ambazo wameshinda kwenye tuzo za ATE 2017.
Akizungumza kuhusu ushindi huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MeTL Group, Hassan Dewji, alisema wamefurahishwa na ushindi huo, lakini pia unaonyesha jinsi gani kampuni inafanya vizuri katika soko la hapa nchini.
"Tuna furaha kushiriki kwenye tuzo za ATE 2017 na tuna furaha kushinda tuzo nne, naamini tumekuwa moja ya kampuni tano ambazo zimeshinda tuzo nyingi. Nafikiri sisi ni moja ya kampuni kubwa nchini na tunaendelea kukua na kugusa maisha ya watu wengi kila siku, ushindi kama huu utuwezesha kuongeza juhudi zaidi," alisema Dewji.
-
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia