Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikaanga kahawa mara
baada ya kutembelea Kitengo cha kukaanga Kahawa katika Ofisi za Bodi ya
Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 16 Disemba 2017. Picha
Zote na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna kahawa
zinazohifadhiwa mara baada ya kutembelea Maabara ya kuandaa kahawa kwa
ajili ya wanunuzi katika Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani
kilimanjaro, Jana 16 Disemba 2017
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo
kuhusu uendeshaji wa mnada wa kahawa kwa mfumo wa kisasa Kutoka kwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Ndg Primus Kimaryo alipotembelea
Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa ziarani Mkoani kilimanjaro, Jana 16
Disemba 2017
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwasili katika chuo cha
mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani
humo, Jana 16 Disemba 2017.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua miongoni mwa
mashamba ya kufundishia kilimo cha mpunga mara baada ya kikao na
watumishi wa chuo cha mafunzo ya Kilimo Kilimajaro (KATC) wakati wa
ziara ya kikazi Mkoani humo, Jana 16 Disemba 2017
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la Kusimamia
sekta ya Kahawa nchini Ndg Primus Kimaryo ameagizwa kusimamia na
kuwalipa haraka wakulima malipo mara baada ya kukusanya mazao yao kwani
kufanya hivyo kutawezesha mazingira mazuri ya biashara na kuwanufaisha
wakulima kutokana na kilimo hicho.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ametoa agizo hilo jana
Disemba 16, 2017 alipotembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa akiwa katika
ziara ya kikazi Mkoani Kilimanjaro.
Mhe
Mwanjelwa alisema kuwa pamoja na wakulima kuuza kahawa kwa bei ya
shilingi 5000 kwa kilo katika msimu wa mwaka 2016/2017 lakini bado
changamoto ni kubwa ya ucheleweshaji wa malipo kwa wananchi jambo ambalo
linarudisha nyuma ufanisi wa zao.
Alisema
miongoni mwa kazi kubwa ya Bodi ya Kahawa nchini ni pamoja na kulinda
maslahi ya wakulima dhidi ya makundi mbalimbali yanayofanya biashara ya
zao la kahawa hivyo kucheleweshwa kulipwa malipo yao ni ishara ya Bodi
hiyo kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.
Aidha,
Kaimu Mkurugenzi huyo wa Bodi ya Kahawa ametakiwa kuwa na mikakati
imara na yenye tija itakayolifanya zao la kahawa kuwa na ubora zaidi
Duniani kwa kwa kuliongezea thamani.
Katika
ziara hiyo pia Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
alitembelea chuo cha mafunzo ya Kilimo Cha Kilimajanro (KATC-Kilimanjaro
Agricultural Training College) ambapo ameupongeza uongozi wa Chuo hicho
kwa kuwawezesha zaidi ya wakulima 7000 katika skimu zaidi ya 100
kuboresha kilimo cha mpunga na mazao mengine hivyo kupata ongezeko kubwa
la mazao.
Sambamba
na pongezi hizo pia amewataka kuongeza ufanisi katika utendaji ili
kuunga mkono kwa vitendo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa
kufanya kazi kwa bidii, ufanisi, na ubunifu.
Aliwasisitiza
wananchi hao kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuwa wabunifu katika
kazi ikiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia