Umoja
wa Mataifa nchini Tanzania umezindua rasmi ofisi zake mjini Dodoma ili
kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamisha makao yake makuu. Ofisi
hiyo, iliyo katika Mtaa wa Mlimwa, Area D, itakuwa na ofisi za mashirika
7 kati ya 23 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania hivi
sasa. Mashirika hayo saba yatakayotumia ofisi hizo ni pamoja na UNICEF,
UNDP, UNFPA, UN Women, IOM, FAO na WHO.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Kassim,
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, ambapo ofisi hizo sasa
ni rasmi kuendesha shughuli za Umoja wa Mataifa kutokea mkoani Dodoma.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith
S. Mahenge, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa
UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez; Mwakilishi wa Nchi wa UNICEF, Bi.Maniza
Zaman, wafanyakazi wa UN, maofisa wa Serikali na wanafunzi walioalikwa
kutoka shule mbalimbali za mkoani Dodoma.
- Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP
nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr.
Augustinew Mahiga na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa Nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Akizungumza
wakati wa tukio hilo; Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
Mkazi wa UNDP, Bw. Rodgriguez, alisema, “Uzinduzi wa ofisi hii
utawezesha na kukuza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Serikali hasa
katika kipindi hiki muhimu Serikali inapohamia Dodoma.
Umoja wa Mataifa hufanyakazi kwa karibu na Serikali, na ofisi hii ni hatua ya kwanza katika Umoja wa Mataifa kuhamia Dodoma.”
- Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine
Mahiga akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi w UNDP Nchini
uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma
Desemba 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Akitoa
shukrani zake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman, alisema mashirika ya Umoja
wa Mataifa hushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono mpango
wake wa maendeleo wa miaka mitano kupitia Mpango wa Msaada wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).
- Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP
nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi yake
uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma
Desemba 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
- Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa
mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne
kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki, Dr. Augustine Mahiga (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
- Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP
nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa
UNDP, Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu).
- Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa
akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
- Waziri
Mkuu,. Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa
mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini, na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
- Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata keki ikiwa ni moja ya shughuli za
ufunguzi wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) eneo la
Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga. (Picha na
ofisi ya Waziri Mkuu).
- Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini , eneo
la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Watatu kushoto waliokaa ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki, Balozi Dr.
Augustine Mahiga na watatu kulia waliokaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Matifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkluu)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia