Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Na Woinde Shizza,Simanjiro
Timu ya jamii ya wafugaji wa Naisinyai S. C ya Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, imeshinda ngao ya maadili iliyoandaliwa na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuifunga
Mirerani SC kwa penalti 6-5.
Katika
mchezo huo wa fainali uliochezwa juzi kwenye uwanja wa barafu mji mdogo
wa Mirerani, mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena
Omary.
Hadi dakika 90 ya
mchezo ulipomalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana na walipopigiana
penalti tano kwa tano hakukuwa na mshindi ndipo wakapigiana penalti moja
kwa moja na Naisinyai ikashinda.
Katibu
Tawala huyo Omary akizungumza wakati wa kukabidhi ngao hiyo ya maadili
kwa timu ya Naisinyai alisema jamii inapaswa kupiga vita matumizi ya
vitendo vya rushwa kwa kila sehemu.
Alisema
jamii inapaswa kuzingatia hilo kupitia kauli mbiu ya wajibika, piga
vita rushwa, zingatia maadili, haki za binadamu na utawala bora kuelekea
uchumi wa kati.
"Tupige
vita rushwa kila mahali, kuanzia michezo ni, makazini, polisi,
hospitalini, mahakamani na kila eneo ukiona rushwa inatumika toeni
taarifa," alisema Omary.
Mkuu
wa Takukuru wilaya ya Simanjiro Mashauri Elisante alisema mashindano
hayo yalishirikisha timu nne za Naisinyai SC, Mirerani SC, Veterani
Mirerani za Simanjiro na Tanzanite FC ya wilaya ya Arumeru mkoani
Arusha.
Alisema lengo la
mashindano hayo ni maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu
kitaifa na kupiga vita vitendo vya rushwa.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Naisinyai, Taiko Laizer alisema hii ni mara ya pili kwa
mwaka huu timu hiyo kubeba ubingwa wa soka kwani awali walishinda kombe
la mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya.
Laizer
alisema siri ya ushindi mara mbili kwa mwaka mmoja kwenye timu hiyo ni
kuzingatia mazoezi, nidhamu na ushirikiano wa uongozi na wananchi kwa
ujumla.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia