Ticker

6/recent/ticker-posts

DCEA WATOA ELIMU KINGA KWA VIJANA KATIKA JUKWAA LA “JIONI YA ZAMANI” ARUSHA

 


 







Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 17.08.2024 imetoa elimu kinga kwa vijana 53 katika Jukwaa la ‘Jioni ya Zamani’ lililofanyika katika Maporomoko ya Napuru _"Napuru Waterfalls"_ wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. 


Elimu hiyo iliyotolewa kwa vijana hao kwa njia ya mdahalo ilikuwa na mada kuu isemayo; *_"Uhusiano wa Ujana na Uraibu wa Dawa za Kulevya"_*.


DCEA Kanda ya Kaskazini ilitumia jukwaa hilo adhimu kuwaasa vijana kutojihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na kutowanyanyapa waraibu walioathirika na matumizi ya dawa hizo badala yake wawaunganishe waraibu hao na huduma za matibabu yaliyopo karibu na mazingira yao wanayoishi.


Post a Comment

0 Comments