Ticker

6/recent/ticker-posts

DCEA waingia katika kampeni ya uokotaji sindano zilizotumika na waratibu wa Madawa ya kulevya

 



Na Woinde Shizza Arusha


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth and Community Rehabilitation (YCR) imeamua kuendesha kampeni maalum ya uokotaji wa sindano mitaani.




Sindano hizo ni zile zimeshatumika na waraibu wa dawa za kulevya na kuzitupa hovyo mitaani kitendo ambacho ni hatari sana kwa mazingira na jamii inayozunguka maeneo hayo kwa ujumla hasa watoto wadogo.






Afisa elimu kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DSEA) Shaban Miraji amesema zoezi hilo maalum lililofanyika katika maeneo ya Darajani, Ngarenaro na Ungalimited ndani ya Jiji la Arusha lina lengo la kuhakikisha jamii inabaki salama dhidi ya madhara yatokanayo na utupaji hovyo wa sindano ambazo zimeshatumika.






Amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano pamoja na kuziwezesha Asasi hizo ili ziweze kufanya shughuli zake za kila siku kwa ufanisi na weledi kwenye jamii hasa zile hatarishi.

Post a Comment

0 Comments