Ticker

6/recent/ticker-posts

DCEA KANDA YA KASKAZINI YATOA ELIMU JUU YA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA JIJINI ARUSHA

 Na Woinde Shizza 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Tanzania Health and Social Services(THSS) tarehe 25.08.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya katika bonanza la August Cup iliyofanyika katika uwanja wa Ilboru Arusha (M).

Aidha, elimu hiyo ilitolewa kwa wanamichezo zaidi ya 60 ikiwa na lengo la kuwapa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya. Elimu hii itawasaidia wanamichezo hao ambao wengi wao ni vijana kutojihusisha na dawa za kulevya sababu zinaweza kuwakosesha utimamu mchezoni na kuharibu ndoto zao za kuja kuwa wachezaji wakubwa baadae.

Pia, wanamichezo hao walihamasishwa kuendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure 119.

Post a Comment

0 Comments