Ofisa ustawi ya jamii kutoka mamlaka ya dhitibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya kaskazini (DCEA)Sara Ndaba wa tatu kushoto akiongea na wananchi waliotembelea katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya 30 ya nane nane yanayofanyika njiro ndani ya jiji la Arusha
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Katika kuhakikisha matumizi ya madawa ya kulevya yanaisha kabisa kama sio yanapungua mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya kaskazini wameteketeza jumla ya magunia 173 ya bangi na kuna kesi 36 zimefunguliwa .
Hayo yamebainishwa na ofisa ustawi ya jamii kutoka mamlaka ya dhitibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya kaskazini (DCEA)Sara Ndaba wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya 30 ya nane nane yanayofanyika njiro ndani ya jiji la Arusha ambayo kauli mbiu yake inasema chagua viongozi bora wa serikali za mitaa Kwa maendeleo endelevu ya kilimo mifugo na uvuvi.
Aidha aliwataka wakulima ambao wanalima vilimo vya madawa ya kulevya aina ya bangi na mirungi kuacha mara moja kwani ni haramu na kunasheria imeundwa Kwa ajili ya kuwakamata wale wote ambao wanalima na hatua kali zinachukuliwa dhidi yao.
"Katika maonyesho haya tumekuwa tukitoa elimu juu ya adhari za matumizi ya bangi au kilimo cha bangi na pale ambapo mkulima anaweza kuingia vishawishi vya kupata fedha za haraka haraka na kuingia katika Kilimo hicho tunampa elimu asiweze kuingia katika Kilimo hicho maana ni kinyume na Sheria na pale atakapo bainika ataingia kwenye mikono ya Sheria" alisema Sara
Aliwataka wakulima hao ambao wanalima mazao ya madawa ya kulevya waache badala yake walime mazao ya chakula ,mazao ambavyo yanaruhusiwa ambavyo ni yabiashara lakini wasijiingize katika Kilimo Cha bangi au mirungi.
Alisema hadi Sasa wametoa elimu hiyo Kwa wananchi wa vijiji vya kisimiri pamoja na losinoni vilivyopo wilaya ya Arumeru maeneo ambayo yanaongozwa kwa kulima bangi na wamewataka wakulima hao kulima mazao mengine na kuachana na bangi na mirungi .
Alibainisha kuwa wakulima hao walieleza sababu ya kulima mazao hayo kuwa ni ukosefu wa maji pamoja na miundo mbinu ya barabara ambapo alisema baada ya kutoa elimu walienda kufanya tasmini wakiwa na ma ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa na kwenda kuwaeleza namna gani watachanganua matatizo hayo yakiwemo ya barabara pamoja na maji
Aidha alibainisha kuwa katika kuendeleza kutoa elimu mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuel Kaganda pia katika ziara yake akiongea na wananchi hao alitoa wito kwa wananchi hao kulima mazao mbadala kama pareto ambalo ndio zao lingine linaloendana na maeneo hayo na kuachana kabisa na kilimo cha bangi ambacho ni hatari kwa wananchi wengine ambao wanaenda Kutumia.
Tags
HABARI MATUKIO