Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUTANO WA 59 WA WAJUMBE WA BODI YA ESARBICA WAKUTANA ARUSHA

Katika mkutano wa 59wa bodi ya wakurugenzi wa uhifadhi wa nyaraka za serikali kutoka nchi za mashariki na kusini mwa wsafrika ambao umeanza Leo jijini Arusha .


Akifungua kikao icho katibu mkuu ofisi ya ofisi ya Rais utumishi Xavery daudi amesema nyaraka hizo nimuhimu kwamanufaa ya nchi ndiyo maana serikali imehimza mfumo wa matumizi ya Teknolojia.

Amehimiza taasisi na nchi wanachama kuwa na wataalamu wazawa na wazalendo .

Kwa upande wa mkurugenzi kutoka ofisi ya Rais idara yakumbukumbu na nyaraka za Taifa Firmini Msiangi amesema bodi hiyo imeanzishwa mwaka 1969 ambapo umehusisha nchi 14 kati ya nchi 15 ambapo watajadiliana namna yauboreshaji nyaraka kutoka kwenye makaratasi kwenda kidigitali ili kuimarishwa kwa huduma bora kwa wananchi na serikali katika kuhakikisha inaleta mabadiliko.

Hata hivyo bodi hiyo imekua ikikutana kila mwaka ambapo kwa mwaka huu wamekutana jijini Arusha kwa siku 3 ikiwemo kujadiliana na kupeana uzoefu juu ya namna bora ya utunzaji wa nyaraka.




Post a Comment

0 Comments