MAKONDA MKUU WA MKOA WA ARUSHA AREJEA KAZINI NA KUANZA KITEKELEZA MAJUKUMU YAKE

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paul Makonda, hatimae Leo amerejea jijini Arusha kuendelea na majukumu yake ya kikazi.


Makonda amekuja Leo baada ya kutokuonekana hadharani kwa  zaidi ya mwezi mmoja na  kuibua minong'ono mingi kwenye mitandao ya kijamii,kwa kile kilichodaiwa alinyweshwa sumu huku wengine wakidai alikuwa likizo.

Mara ya mwisho Makonda alionekana Julai 14, 2024 katika mashindano ya pikipiki ya Samia Motorcross Championship yaliyofanyika katika viwanja vya lakilaki,eneo la Kisongo, Mkoani Arusha.



Leo Ijumaa Agosti 16,2024 Makonda amekuja na kuanza kazi kwa  kutembelea na kukagua ukarabati wa jengo la kupokea wageni wanaowasili na kusubiri kuondoka ulioko Kisongo.

Baada ya ujio wake aligoma kuelezea alipokuwa zaidi ya  kuagiza ukarabati wa jengo ukamilike kwa wakati ambayo ni Septemba Mosi,2024 .



Meneja wa uwanja huo, Godfrey Kaaya, amesema jengo hilo lililofikia asimilia 90,  hadi hadi kukamilika kwake litagharimu Shilingi 8.0 .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post