BAJETI KUU YA SERIKALI YAPITISHWA RASMI MJINI DODOMA



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma, walipotembelea bungeni mjini Dodoma, siku ambayo Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Sh. trilioni 31.7 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James (wa nne kulia-mbele), akiongoza Vongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango kufuatilia tukio la Wabunge wakipiga kura kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Chakwa-Zanzibar, Mhe. Bhagwanji Meisuria (katikati), na mkewe Kissum Biin Bhagwanji Meisuria, wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Charles Kitwanga akimkumbatia kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Mnauye akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), akimpongeza kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiteta jambo na maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipongezwa na Askari wastaafu wa Jeshi la KAR waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939-1945 baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Shilingi trilioni 31.7 mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kwa ushirikiano mkubwa aliompatia hadi kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa na kusimamia Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7 iliyopitishwa na Bunge kwa kishindo mjini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post