“Ujana ni rika, ujana ni wakati na wakati haurudi nyuma”
haya yalizungumzwa na mgeni rasmi Ndg. Rodrick Mpogoro Naibu katibu
Mkuu CCM Bara kwenye mahafali ya Vijana Chama Cha mapinduzi kutoka Vyuo
na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo 28/05/2017 katika
ukumbi wa King Solomoni Kinondoni.
Ndg.
Rodrick Mpogoro alisema, Siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyote
inategemea namna anavyotazama na kutathmini mambo. Ni mtazamo chanya
pekee ndiyo humvusha mtu kwenye mafanikio, hivyo ipo haja kwenu vijana
kujikita kutazama fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu ili
kujitengenezea vipato vyenu wenyewe kuliko kusubiria ajira, alisema.
"Sura
ya Chama Cha Mapinduzi inajengwa na wanachama wenyewe kwa vitendo,
jengeni uadilifu, zungumzeni habari ya uzalendo wa nchi yenu, jengeni
maslahi kwa wanyonge, jifunzeni historia ya Chama, someni katiba na
kanuni zake, fanyeni kazi kwa bidii na jengeni moyo wa kujitolea
mkifanya hayo mtafanikiwa. Alisema.
Akiendelea
kuhutubia hadhara, Ndg. Mgeni rasmi alisema, ni vyema kwa wanachama,
wananchi na kila mpenda amani, umoja na maendeleo ya Taifa kuendelea
kumuunga mkono Rais wetu Mhe Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi
anazozifanya za kupambana na ubadhilifu wa mali za umma kwani anaiishi
misingi ya Chama Cha mapinduzi kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni yake
kupitia katiba Ibara ya 5. "Simameni imara katika kumuunga mkono Rais
wetu kwani anaiishi misingi ya Chama Cha Mapinduzi katika kujenga
uzalendo wa nchi".
Mahafali hayo
yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Ndg. Shaka Hamdu
Shaka K/Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),
Ndg. Daniel Zenda K/Katibu wa Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM, Uongozi wa
Senate Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam na makada kutoka vyuo
mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam.