“MEYA JIJI LA TANGA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WAJASIRIAMALI KWENYE KATA 27”


  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na wakina mama wajasiriamali kwenye kata ya Nguvumali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo aliyaandaa kwa ajili ya kukabiliana na fursa mbalimbali za kujiwekeza kiuchum ambapo mafunzo hayo yatafika kwenye kata 27 za Jiji hilo
 Baadhi ya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Nguvumali Jijini Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
WANAWAKE wajasiriamali Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utengenezaji na ubinifu wa bidhaa mbalimbali ili waweze kujikwamua kichumi jambo ambalo litasaidia kuondokana na utegemezi kwenye jamii.

Mafunzo hayo ambayo yamekwisha kuanza katika kata ya Nguvumali yanatarajiwa kuwafikia wanawake wajasiriamali 120 na baadae kuendelea kwenye maeneo mengine katika Jiji la Tanga.

Akizungumza juzi wakati akifungua mafunzo hayo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema mpango huo utasaidiakuwakomboa wanawake kiuchumi lakini pia kuwaandaa na ujio wa miradi mikubwa miwili mkoani hapa ikiwemo wa bomba la mafuta na kiwanda kikubwa cha kuzalishia saruji.

Alisema pia licha ya kuwapa uelewa masuala hayo lakini namna bora ya kuzitumia kwa malengo yatakayokuwa na tija fedha wanazokopa kutoka kwenye taasisi za kibenki kwani baadhi yao wanashindwa kutambua wazitumie vipi na kuzirejesha.

“Utakuta wakina mama wajasiriamali wanakopa fedha kwenye taasisi mbalimbali kwa malengo ya kufanya biashara lakini kutokana na kutokuwa na elimu hivyo wanaishia kuzitumia kwenye mambo mengine na kusababisha madeni “Alisema.

“Lakini pia wanawake wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa ya mafunzo hayo kuweza kujiongezea wigo mpana kwani ujio wa mradi wa bomba la mafuta wenzetu wanaokuja kutoka nchini Uganda hivyo lazima waweze na uwezo wa juu “Alisema.

Aidha pia alisema wanatumia nafasi hiyo kuwaandaa kwa kusaidia ili waweze kujiandaa kwa kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mboga mboga na matunda ikiwemo uuzaji wa mayai.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Kata ya Nguvumali ,Saumu Omari mafunzo hayo yamewaongezea maarifa ambayo wanaweza kuyatumia ili kuweza kuongeza uzalishaji lakini pia kukabiliana na soko la ushindani wa bidhaa.

Alisema kupitia elimu hiyo ya ujasiriamali wanaweza kuona namna gani bora ya kuanzisha na kubuni miradi ya kuwainua kiuchumi kwa kuzitumia fursa zitakazo patikana
kutokana kwa kuwawezesha kukuza kipato chake.

 Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post