Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kigongo feri
Wilaya ya Misungwi, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea
Chato kwa ziara ya siku mbili Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja
Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga wakati alipowasili mjini Chato mkoani
Geita Juni 21, 2017 kwa ziara ya siku mbili mkoani humo. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika swala ya magaharibi katika
futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu mjini Chato, mkoani Geita, Juni 21,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akifuturu pamoja na Askofu Mussa Magwesera wa
Kanisa la African Inland Church (AIC) Dayosisi ya Geita (kushoto) na
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alhaj Yusuph Kabaju(kulia) katika futari
iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli,
mjini Chato, mkoani Geita Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)