Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Balozi
Mstaafu Ali Abeid Karume amesema uamuzi wa mdogo wake wa kike kuhama
CCM na kujiunga CUF hakuutegemea hivyo amemsihi ni vyema akautumia
ubini wa jina la mumewe kuliko kuendelea kulitumia jina la hayati Sheikh
Abeid Amani Karume akiwa upinzani.
Amesema
Mzee Katume katika maisha yake alipingana na wapinzani na usuktan
uliowakandamiza waafrika katika visiwa vya Unguja na Pemba hadi
yalipofanyika Mapinduzi mwaka 1964 hivyo mwanawe yeyote kwenda upinzani
ni mambo ya kushangaza.
Balozi
Karume ameeleza hayo jana mjini unguja katika mahojiano maalum kufuatia
uamuzi wa mdogo wake wa kike aitwaye Aksa Abeid Karume kuhama CCM na
kujiunga na CUF .
Alisema
anaelewa fika kwamba mdogo wake bila shaka atakuwa amezidiwa nguvu za
ushawishi toka kwa mumewe amaye amewahi kuwa mgombea mwenza wa urais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia cuf Nassor Khamis Mohamed.
"Sikutegenea
kumsikia mdogo wangu Aksa akipitisha uamuzi huu, pamoja na kuwa ana
uhuru wa kuchagua lolote, amechagua jambo ambalo halina asili wala
mnasaba na familia ya baba yetu" Alisema Balozi Karume.
Aidha
Balozi huyo mstaafu ambaye ni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa SMZ,
alisema mara nyingi wanawake wanapoolewa hutumia majina ya waume zao
hivyo itakuwa busara kwa Aksa akatumia jina mumewe na kuacha la m
Mzee Karume.
Alipotakiwa
kueleza uamuzi huo umeiathiri kwa kiasi gani familia yao, Balozi huyo
alisema heshima ya Mzee Karume itaendele kubaki mahali pale pale na wala
haitavunjika kwa sababu tu miongoni mwa mwanawe atahama ccm na kwenda
upinzani.
"Heshima ya
Mzee wetu haitavunjika kwa mtoto au mjukuu wake yeyote kujiondoa CCM na
kwenda upinzani, Mzee aliyatoa muhanga maisha yake kuwatetea wananchi
wanyonge hadi wakapata uhuru na ukombozi kamili, tunaojua na kufahamu
kamwe hatutayumba "Alieleza Balozi huyo .
Balozi
huyo alikosoa hatua ya kaka yake ambaye alikuwa Rais Dk Amani Karume
kumpa uwaziri Mansoor Yussuf Himid huku akijua babu yake marehemu
Mohamed Sakum jina ndiye aliyekuwa katibu Mkuu wa ZNP kilichokuwa
kikishindana kisera na ASP kuelekea uhuru wa Zanzibar dhidi ya ukoloni.
"Sikuzishangaa
kedi na ukorofi wake dhidi ya sera na misimamo ya ccm ukifanywa na
Mansoor hadi akafukuzwa CCM, mapema nilishtuka kusikia amepewa uwaziri
na shemeji yake, kujiunga kwake CUF na kuipinga CCM ni jambo
lililotegenewa "Alisisitiza Balozi Karume.
Hata
hivyo Balozi huyo mstaaafu ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM
alisema CCM ni taasisi kamili ya kisiasa hivyo haiwezi kudhoofika au
kufa kwasababu tu mtoto mmoja au wawili wa mwanamapinduzi yeyote au
Jemedari wa Mapinduzi kujiondoa na kujiunga upinzani .
Pia
alieleza kuwa yeye na watoto wake wataendelea kubaki CCM huku wakijua
huwezi kuitaja CCM bila kuvitaja TANU na ASP na ASP ndicho chama
kilichoongozwa na hayati Mzee Abeid Karume hatimaye akawa Rais wa Kwanza
Zanzibar na Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania .
"Mzee wetu kwa
kushirikiana na Mwalimu Julius Nyerere ndiyo waliounda Taifa la
Tanzania.Taifa hili haikuachwa na wakoloni, Ni jipya lililoundwa
kutokana na kuthamini umoja na uzalendo, maarifa na kutazama maslahi
mapana ya kijamii "Alieleza Balozi Karume ambaye ni mtoto wa pili wa
hayati Mzee Abeid Karume .
"Namshamgaa
Aksa mbona wakati kaka yake Amani Karume akiwa Rais hakutangaza kuhama
CCM ,kwanini afanye hivyo sasa, madai ya kusema anaunga mkono harakati
za ukombozi , ukombozi na uhuru kamili wa zanzibar uliletwa na baba yake
kupitia ASP 'Alisema.