RC MAKONDA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA MANISPAA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTONIKI (e-RCS) KUKUSANYA MAPATO


MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizingumza na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Picha Zote na Mathias Canal
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mmbando (Kulia)
Wakurugenzi, Na Maofisa Biashara wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati wa kikao Cha pamoja katika Ukumbi wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama.
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizingumza na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akimsikiliza kwa makini MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama. Mwingine ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagoromjuli
Na Mathias Canal, Dar es salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa Jijini Dar es salaam kujiunga katika mfumo mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (e-RCS) ili serikali iweze kupata kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.
Rc Makonda ametoa agizo hilo leo June 20, 2017 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama,  dhifa iliyohudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Wakurugenzi wa Manispaa sambamba na Maofisa Biashara wa Manispaa zote za Jiji la Dar es salaam.
Mhe Makonda alisema kuwa kujiunga katika mfumo huo Manispaa zote zitapata urahisi katika kuwahudumia wananchi sawia na kurahisisha kuboresha vyanzo vya mapato.
Alisema kuwa mfumo huo utaongeza Mapato katika Manispaa, Kuondoa usumbufu kwa wananchi ikiwemo kuepuka Rushwa, sambamba na Kuimarisha huduma kwa wananchi.
"Najua Kuna watu Jambo hili litawakwaza Sana hususani wale wapiga dili lakini niwahakikishie kuwa kuna umuhimu mkubwa Sana kujiunga na Mfumo huu wa kisasa wa kuhifadhi kumbukumbu kwani ni njia rahisi ya kutoa taarifa pia ni Mfumo mzuri kwa usalama wa Taifa" Alisisitiza Mhe Makonda
Wakurugenzi hao wameagizwa kutumia wiki moja kujadili namna gani ya kujiunga na Mfumo huo huku akielekeza Hadi kufikia Agosti Mosi mwaka huu Manispaa zote ziwe zimejiunga na Mfumo huo.
Aidha, Alisema kuwa Kujiunga na Mfumo huo wa serikali wa ukusanyaji Mapato kwa njia ya Kielektroniki itarahisisha umakini wa huduma hivyo kuachana na Mfumo wa zamani wa kutuma watu kutambua watu ambao leseni zao zimemaliza muda wa matumizi.
Alisema kuwa Jiji la Dar es salaam Lina vituo vya Daladala zaidi ya 800 hivyo endapo kama ukiwekwa mfumo mzuri wa ukusanyaji wa Mapato katika vituo hivyo itakuwa ni chanzo Cha upatikanaji wa mapato ya serikali.
Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki ulizinduliwa June Mosi Mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John pombe Magufuli ambaye aliambatana na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post