Jamii mji
mdogo wa Matui wilayani kiteto imeaswa wawe wepesi katika utekelezaji wa
shughuli za maendeleo zitakazosaidia ukuaji wa maendeleo na hivyo kuweza kupata
huduma muhimu kwa jamii hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Diwani wa kata ya Matui Kidawa Athman Iyavu wakati akiongea na
wanahabari waliotembelea kata hiyo kujionea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na
halmashauri pamoja na nguvu za wananchi.
Alisema kuwa
ilikufikia malengo ya mji mdogo lazima wananchi na viongozi wakafanyakazi kwa
ushirikiano utakaosaidia kumaliza miradi kwa wakati ikiwemo mradi wa wodi pacha
za kinamama,watoto na Chumba cha upasuaji ili kuweza kupata hadhi ya kituo cha
afya.
“Nawasihi
wananchi wangu hapa matui tuwe wepesi katika kuchangia maendeleo yetu
tukisaidiana na serikali kuhakikisha tunafikia kwenye mafanikio ya upataji wa
huduma bora za Afya bila kutembea umbali mrefu” asisitiza Iyavu
Nae Mtendaji
kata ya Matui Zainab Mahiza alisema kuwa mradi huo hadi kukamilika utagharimu
kiasi cha milioni 100 na hadi sasa zimetumika kiasi cha million 37 ambapo
halmashauri imechangia milioni 23 na wanachi wamechangia milioni14.5 ambapo
mpaka sasa wodi mmoja imepauliwa na wanasubiria fedha za ujenzi wa awamu ya
pili.
Alisema kuwa
kutokana na ukosefu wa fedha mradi huo haujakamilika kwani jamii yetu
inategemea kilimo kujipatia riziki na fedha na msimu huu haukuwa mzuri hata
shughuli za maendeleo zimekwama kutokana na hali hiyo.
“Nawasihi
wananchi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa chakula hicho kidogo mkitunze
ilikiweze kuwasaidia kuendesha maisha pia wafugaji wenye mifugo wauze michache
kuwezesha kununua chakula kwa akiba yao” alisema Mahiza
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia