BREAKING NEWS

Friday, October 6, 2017

Mdori Fc yatwaa ubingwa kombe la kupiga vita ujangili .RC Manyara aagiza timu zote kusajiliwa



Mwandishi wetu

Arusha.Timu ya soka ya Mdori Fc ya wilayani Babati  mkoa wa Manyara juzi, imetwaa ubingwa wa michuano ya Chemchem Cup ya kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori na kupiga vita ujangili baada ya kuichapa timu Manyara Fc magori 2-1.

Kutokana na ubingwa huo, timu hiyo ilipewa zawadi ya fedha taslim 1.4 milioni  na kikombe vilivyotolewa na wadhamini wa michuano Chemchem Lodge, ambapo timu 23 zilikuwa zikishiriki.

Katika mchezo huo wa fainali, ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendela, timu ya Manyara Fc ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 34 lililofungwa na Hamad Nassaro.

Mdori wakicheza kwa kuelewana walisawazisha goli hilo dakika ya 37 gori ambalo lilifungwa na  Ally Mido  kwa shuti kali baada ya kuitoka ngome ya Manyara Fc.

Kipindi cha pili, Mdori walikianza kwa kasi na katika nadakika ya 59, Ally Mido tena alifunga gori la pili baada ya kuwahada kwa chenga walinzi wa Manyara Fc.

Akizungumza baada ya kukabidhi vikombe na zawadi, mkuu wa mkoa, Bendela ambaye kitaaluma ni kocha, alisema ameshuhudia vipaji vikubwa kwa timu zilizocheza fainali.

Alisema ili kuyapa hadhi mashindano hayo, ambayo lengo lake la kuhifadhi wanyamapori katika eneo la hifadhi ya jamii ya burunge, timu zote 23 zinazoshiriki zinapaswa kusajiliwa.

"nawaagiza viongozi wa chama cha soka mkoa wa manyara mliopo hapa mzisajili timu zote zilizoshiriki mashindano haya ili yawe rasmi baadaye tupate timu moja ya mkoa"alisema

Bendela pia alieleza kumshukuru mkurugenzi wa Chemchem foundation, Nicolaus Negre na watendaji wengine kwa kuanzisha mashindano hayo.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi, Negre alisema lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha uhifadhi nakupiga vita ujangili.

"kama mkitaka tuendelee na mashindano haya, lazima tupambane na majangili ili wageni waendelee kuja kwenye eneo letu la hifadhi ya jamii wanyamapori burunge"alisema.

Washindi wa pili wa michuano hiyo, walipewa kikombe na fedha raslim sh 1 milioni, mchezaji bora nakipa bora walipewa zawadi ya sh 25,000 kila mmoja sawa na timu yenye nidhamu.

Kwa upande wa mpira pete,timu ya Sangawe Fc ilitwaa ubingwa na kuzawadiwa sh 500,000.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates